Hili sharti linaiweka rehani ndoa yangu

Hili sharti linaiweka rehani ndoa yangu

Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2,304
Reaction score
780
Kama mtakuwa mnakumbuka niliwahi kuwaletea habari inayohusu uhusiano wangu na mdada flani ambae ckuwa na mipango ya kumuoa na hata nilipomwambia nataka kuoa alinipa 'go ahead' huku akisema atamuheshimu mke wangu.

Lakini ikawa kinyume chake, siku moja wakakutana kwny kitchen party, akaanza kuomba nyimbo zenye maudhui ya vijembe kwa wife, kwa kuwa wife alikuwa keshatonywa na wapambe nux kuhusu chezo lote basi cku hiyo alimpa kipigo cha kutosha na aliporudi home hata hakuniambia chochote kilichotokea.

Twende kwenye stori kamili sasa;

Juzi nilikuwa na miadi na hako ka mchepuko,nikatunga uongo wee hadi ukapatikana, nikamwambia wife naenda mcbani uongo wangu ukatiki nikauseti mchepuko twende tukalale hotel flani, mambo yakawa poa.
Sasa wakati tuko pale hotel tunapata vinywaji si akatokea mama mmoja anaishi jirani yetu ni muongo muongo hivi, akaenda kuunguza picha yote kwa mamsapu.

Sasa niliporudi jana ndio nikakutana na kimbembe nikakuta mwanamama kachachamaa, povu limemtoka, bila simile akawa anaongea kwa jazba, akiwa na hasira zile zile ndio akanipa sharti hili:- nakwambia (akanitaja jina langu, hicho ndio kipimo cha kukasirika kwake ni kunitaja jina) kama hautakwenda kupima UKIMWI hautaingiza hilo dubwasha lako humu akiwa na maana kwamba kuanzia jana mgegedo wangu na papuchi yake havitakuwa na mawasiliano tena.

Hapo ndio ninapopaogopa, kupima huwa sio tatizo sana,lakini shida inakuja kwenye kukubaliana na majibu tofauti na yale yanayopendwa na wengi nikikumbuka kuna jamaa flani kwa hiyari yake mwnyw tena bila kushurutishwa na mtu alikwenda kupima ngoma ( maana nae alikuwa ni mpigaji sana) akaja kupata majibu kwamba hana ukimwi wee jamaa alifurahi kupita kiasi, maana kwa maelezo yake ya awali ni kwamba hajawahi kupima hiyo kitu tangu aanze pilika za kugegeda.

Mwisho wa ile furaha yake jamaa akafa akiwa usingizini.Kinachoniogopesha mimi kupima ni:- ule muda wa kusubiri majibu huwa ni mgumu sana, lakini pia yanaweza kutoka majibu mabaya, au yakiwa mazuri nahofia kufa kwa furaha kama yule jamaa yangu.

Hebu mnishauri jamani nifanyeje kwa hili
 
Nenden wote mkapime mkuu kwa maana kama umeupata asilimia kubwa nae atakua nao? Asikutishe bwana na hizi mvua hz mwenyewe atakuita zile zilikua hasira tu....

Nb. Uache kuchepuka na kama ukifanya hvyo isiwe mbich mkuu ndio maana unapata mawazo ya kupima sa hv
 
Mshauri mkapime wote. Kama wewe ni mchepukaji mkongwe na kama tayari umeambukizwa basi na yeye anahitaji kujua afya yake. Ila post namba 2 hapo juu imekutendea haki
 
Mwanaume yeyote ambae hachepuki na awe wa kwanza kuninyooshea kidole cha kunilaumu
 
nabaki kucheka tu kwa mambo unayofikiria, yaani kichwa chako sijui kinawaza au kinaona madudu yanapita usoni mwako... Endelea na mgegedo tu wala usirudi kwa mke mkubwa.
 
Mshauri mkapime wote. Kama wewe ni mchepukaji mkongwe na kama tayari umeambukizwa basi na yeye anahitaji kujua afya yake. Ila post namba 2 hapo juu imekutendea haki

Imenitendea haki kunitusi!!
 
nabaki kucheka tu kwa mambo unayofikiria, yaani kichwa chako sijui kinawaza au kinaona madudu yanapita usoni mwako... Endelea na mgegedo tu wala usirudi kwa mke mkubwa.

Nisirudi ili iweje sasa
 
Back
Top Bottom