Hili ni suala nyeti, tulitadhimini kwa mapana.

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
1,314
Ni wasiwasi na hofu imejaa katika jamii. Wapo ambao hawaamini lakini wapo wenye kuamini pia. Taarifa hizi zimeifanya taasisi inayoitwa ndoa kuyumba. Mkemia mkuu katupa jiwe GIZANI. Taarifa aliyoitoa ni kwamba katika watu walioenda kupata huduma za DNA juu ya watoto, 49% ya wababa "wamebambikiwa" watoto.

Hili limedhihirisha kwa kiwango kikubwa "UNAFIKI WETU" kwani wakati haya yakitokea nyumba za ibada zinazidi kujengwa na kufulika waumini na wafuasi.

Suala la mahusiano na Ndoa limekuwa ni tete kweli kweli. Ni sawa na ule msemo "alieuza cheni kauza cheni bandia na alienunu katoa pesa bandia"
 
Back
Top Bottom