Hili ndio jukumu pekee walilojipa generation samia

Hili ndio jukumu pekee walilojipa generation samia

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
843
Reaction score
1,024
HILI NDIO JUKUMU PEKEE WALILOJIPA GENERATION SAMIA

Mkurugenzi na Mratibu Taifa wa Taasisi ya Generation Samia, Omari Kimweri Kibanga, amesema kuwa jukumu kuu la taasisi hiyo ni kuyaunganisha makundi mbalimbali na fursa zinazotengenezwa na uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika Kongamano la Wazi la Fursa za Uchumi lililofanyika katika Ukumbi wa Kwatunza Beach, Mwanza, Kibanga alisisitiza kuwa Generation Samia ni kizazi cha mafanikio kinacholenga kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kina kuhusu fursa zilizopo, hasa kupitia mfumo wa NeST unaohusiana na mgao wa 30% wa Samia kwa vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu.

“Sisi kizazi cha mafanikio (Generation Samia) tumejipa jukumu moja tu – kuyaunganisha makundi mbalimbali na fursa zinazotengenezwa na uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya mama yetu mpendwa, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi 2025-2030, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Kibanga.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na zaidi ya watu 8,000 kutoka sekta na makundi mbalimbali, likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu fursa za kiuchumi zinazopatikana kupitia sera na mipango ya serikali.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, huku Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Ndg. Denis Simba akihudhuria kwa ajili ya kutoa mada na mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa NeST na fursa zilizopo kwenye mgao wa 30%.

Kwa mujibu wa Kibanga, Generation Samia itaendelea kutoa elimu na kuwa kiungo kati ya wananchi na serikali ili kuhakikisha kila mtu anafaidika na fursa zinazotolewa.
@gen_samia
#GenS
#KizazicChaMafanikio
#ConnectionYaTendaZaSerikali
 

Attachments

  • VID-20250401-WA0860(1).mp4
    59.6 MB

Similar Discussions

Back
Top Bottom