pole sana..........
inaelekea ulizama haswa mapenzini, kumfuatilia mtu miaka 2 si mchezo, na inaonyesha ulipenda kwa dhati, lakini bahati haikuwa yako....
kama mdada alivyokwambia alikuwa kachumbia, uliyafumbia macho yote hayo kwa sababu ya mapenzi.... na usikute alipokwambia ana mtu kamtolea mahari, yupo masomoni ukadhani mdada hayupo serious kwa sababu tu hujawahi kumuona na mtu wala kupata habari zake, kumbe dada wa watu alikuwa anajitunza kwa ajili ya mchumba wake wewe ukadhani hayupo serious au analeta pozi za'kike?"
ila yote hayo ni maisha, huyo dada na mchumba wake wanapendana, mpaka mwanamke kajitunza miaka yote kumsubiria mtarajiwa yake........ na kwa mwanamke ajayejiheshimu hawezi kutoka na wewe ilhali anajua huo ni mtego.....
pia inawezekana alimpa mtarajiwa wake namba yako baada ya kuona upo serious zaidi, au kila akikuambia nae mtu wake bado wewe unamng'ang'ania, au kumfutilia kwako(kumbuka miaka 2 ni mingi) kumegeuka kero kwake, au ameona ndo njia muafaka ya kukufanya umuache awe na amani......
ofcourse maumivu ni makubwa, ukizingatia umewekeza hisia zako hapo...
lakini huo si mwisho wa dunia, kwenye maisha huwezi kupata kila ukitakacho .....
kwanza kubali hali halisi kuwa huyo dada tayari "keshawahiwa"
jitahidi umuone ni wa kawaida
punguza kumpigia simu
punguza kumuona
muepuke
go ut jichanganye na marafiki
in time utamsahau..... si rahisi kama unavyodhani lakini wanasema "time heals"
kwa wakati utajikuta unazoea
kwa wakati utajikuta unamsahau, hata ukimuona kiroho hakitashtuka.... na mwisho wa siku utamchangia sendoff take na kuhudhuria harusi
na mwisho wa siku utampata wako.... wako peke yako....
nakutakia christmass njema.....