Fundi mahiri wa Ujenzi
JF-Expert Member
- Dec 10, 2012
- 4,724
- 3,701
ni nini hizi![]()
Hizo nyingi ni United States Dollars na hizo nyekundu zinaonekana chache ni Tanzanian Shillings
ni nini hizi![]()
Hizo nyingi ni United States Dollars na hizo nyekundu zinaonekana chache ni Tanzanian Shillings
ngoja nikutafte tugawane ma dolale......
wanasemaga maiti alikuwa na roho nzuri,hakuwa mchoyo etc.......
sijawahi kuona wakisifia eti marehem alikuwa na umbo la kuvutia
life is Short ni kweli mwenzio sijawahigi kuona wala kusikia hivyo ati!!!!!!!!!habibi Umenifurahisha haha ha quote zako Muruwa na pekee!!
Wansemaga kuwa Waswahili wazuri wale walokufaga !!life is Short ni kweli mwenzio sijawahigi kuona wala kusikia hivyo ati!!!!!!!!!
Ni kweli,mtu anajidai ana kazi nzuri,ana piga mizinga watu,anapenda muda wote awe na maisha makubwa huku wazazi wakiwa na maisha ya ajabu kijijini.kuna watu humu wazazi wao inawezekana hawataona wajukuu zao/ wanaoweza kuwasimulia wao walikuwa wanaishi vipi,Vijana wa siku hizi ndo maana tunakufa mapema..Hatuwajali wazazi tunaendekeza sana starehe...
Mungu amekubariki umepata kazi nzuri angalau,mkumbuke mama yako japo umbadilishie Kitenge chake kilichochakaa..Mkumbuke Babako japo na kiatu,kila akikivaa ajisikie kweli ana mtoto...Kumbuka wadogo zako japo na Uniform mpya uwapunguzie mzigo wazazi kwa vitu vidogo vidogo..
Sasa wewe ni Bar tu,Bata tu,kila mahali unajifanya we ndo wewe wakati wazazi wamekusomesha kwa shida,walijinyima ili uwe na maisha mazuri,umewasahau..
Unajidai wa kishua sana mtaani wakati nyumba yenu imeezekwa na bati la msaada limeandikwa KORIE mafuta bora ya kupikia na kenchi za miti...Kumbukeni mlikotoka,kidogo ulichonacho jaribu ku-improve maisha ya nyumbani kwenu.
Wazazi wakikubariki hata mambo yako yatakunyookea.,Tunakosa baraka hivi hivi kwa kujifanya wajuaji..Ushauri tu wa Bure...Love your parents.........