Hili nalo neno

Hili nalo neno

Binti1

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2013
Posts
668
Reaction score
1,764
Vijana wa siku hizi ndo maana tunakufa mapema..Hatuwajali wazazi tunaendekeza sana starehe...
Mungu amekubariki umepata kazi nzuri angalau,mkumbuke mama yako japo umbadilishie Kitenge chake kilichochakaa..Mkumbuke Babako japo na kiatu,kila akikivaa ajisikie kweli ana mtoto...Kumbuka wadogo zako japo na Uniform mpya uwapunguzie mzigo wazazi kwa vitu vidogo vidogo..

Sasa wewe ni Bar tu,Bata tu,kila mahali unajifanya we ndo wewe wakati wazazi wamekusomesha kwa shida,walijinyima ili uwe na maisha mazuri,umewasahau..

Unajidai wa kishua sana mtaani wakati nyumba yenu imeezekwa na bati la msaada limeandikwa KORIE mafuta bora ya kupikia na kenchi za miti...Kumbukeni mlikotoka,kidogo ulichonacho jaribu ku-improve maisha ya nyumbani kwenu.

Wazazi wakikubariki hata mambo yako yatakunyookea.,Tunakosa baraka hivi hivi kwa kujifanya wajuaji..Ushauri tu wa Bure...Love your parents.........
 
Nakubaliana na wewe..mtu mjini anatesa,anaishi kwenye nyumba ya kupanga ya kifahari,simu za garama,ma ipad,cjui ma nini nini,mkoko wa kiaina,kumbe home hata kajumba ka Gebo hana..akienda nyumbani na familia wanalala guest kama sio kwa jirani,wengine wanabebaga mahema wakienda kijijini kwao..wengine hata watoto hawajawai kukanyaga kwa babu isitoshe babu bado yupo..mwisho wa siku akifa,atasikia tunazikia makaburi ya kinondoni!wakati uwezo wa kusafirisha mwili upo na wazazi bado wazima..tusijisahau jamani,home is home
 
Kweli lakini saa nyingine muhimu kukumbushana na kuwekana sawa...wakaka wako radhi ahonge mwanamke asimuache kuliko kumnunulie mama ake kitenge au kuliko kumnunulia mdogo wake hata viatu vya shule!Wadada ndo usiseme.....anunue weaving ahakikishe hakuna fashion ya mjini inampita sio ya nywele,viatu,pochi wala nini anaona ajipendezeshe kwanza ndo amnunulie......chenchi atume kijijini.
Hapo wakati mtu unasomeshwa wazazi walijinyima weeee ili mtoto usome na usikose pocket money sasa ivi mmmmh.....Mungu atusaidie vijana aiseee japo sio wote wapo hivyo ila muhimu kukumbushana
 
Vijana wa siku hizi ndo maana tunakufa mapema..Hatuwajali wazazi tunaendekeza sana starehe...
Mungu amekubariki umepata kazi nzuri angalau,mkumbuke mama yako japo umbadilishie Kitenge chake kilichochakaa..Mkumbuke Babako japo na kiatu,kila akikivaa ajisikie kweli ana mtoto...Kumbuka wadogo zako japo na Uniform mpya uwapunguzie mzigo wazazi kwa vitu vidogo vidogo..

Sasa wewe ni Bar tu,Bata tu,kila mahali unajifanya we ndo wewe wakati wazazi wamekusomesha kwa shida,walijinyima ili uwe na maisha mazuri,umewasahau..

Unajidai wa kishua sana mtaani wakati nyumba yenu imeezekwa na bati la msaada limeandikwa KORIE mafuta bora ya kupikia na kenchi za miti...Kumbukeni mlikotoka,kidogo ulichonacho jaribu ku-improve maisha ya nyumbani kwenu.

Wazazi wakikubariki hata mambo yako yatakunyookea.,Tunakosa baraka hivi hivi kwa kujifanya wajuaji..Ushauri tu wa Bure...Love your parents.........

Asante kwa kutukumbusha na hongera kwa kujaaliwa coz nikiitazama avatar yako duu ni nouma
 
kwani lile la kwetu la mifuniko la mapipa umeshalitoa baada ya kupata kazi? juzi na kuktana na kakako mkubwa anasema umeondoka home kabisaaa eti uswahilini...! usifanye hivyo!
 
ila nawe fanya kweli hayo uliyo yaandika kwa familia yako isije ikawa ya nyani asiye ona ......yake
 
ni nini hizi
avatar112514_3.gif
 
Back
Top Bottom