Hili nalo linanikera sana...

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353


Jana nilikua nabrowse instagram nikaona picha ya madawati ambayo yametolewa kama msaada na mmoja wa ma supermodo wetu kitu ambacho sipingi kuwa ni jambo zuri sana lakini kilichonikera madawati yale yalikua na miandishi mikubwa sana kwa mbele 'DONATED BY.....(JINA LAKE). Sasa nikajiuliza kuna ulazima gani aandike jina lake pale tena kwa ukubwa ule? Kwani angeyatoa kimya kimya au kuweka kijichata kidogo tu angepoteza chochote? Anapromote nini?

I can undestand makampuni yakiweka chata zao kwa kuwa wanapromote biashara lakini suala la ukubwa wa maandishi kama hayo hapo juu limekua likinikera sana na pia naona ni some kind of disruption kwa wanafunzi. Na pia in the past nimewahi kuona madawati yaliyokua donated na kampuni ya sigara na makampuni ya bia na yameandika kwa ukubwa kabisa yalikotoka, kwanini wanaruhusiwa kupromote hivi vitu kwa watoto wa shule za msingi?

Angalizo: Picha hapo juu ni mfano tu, I have nothing against WV.
 
Back
Top Bottom