mwamba c
JF-Expert Member
- Jan 2, 2017
- 690
- 2,362
Ndugu wanajamvi kuna jambo limejitokeza leo na limenipa mashaka kidogo.Pamoja na wafanyabiashara kutozwa michango mingi sana na serikali mfano,leseni ya biashara ambayo ni ya lazima,usafi wa mji ambao ni sh. 50000 kwa mwaka(ingawaje hali ya usafi bado inasua sua),mchango wa sijui mambo ya zima moto(fire)ambao ni 40000 kwa mwaka,bado TRA(compulsory na ni wajibu wa kila mfanyabiashara.Sasa niende kwenye point,leo wamepita watu wa serikali za mitaa wanakusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mwenyekiti wa kata na katika fomu kumeandikwa utoe kadri unavyoguswa lkn cha kushangaza ukitoa kile unachoona ni kiwango chako mfano 1000 au 2000 wakusanyaji wanalalamika na kusema ni kidogo sana,je kikubwa ni kipi na kinapimwaje?je serikali kuu haitambui wenyeviti na kuandaa mazingira mazuri ya kazi kwaajili yao?kodi tunazolipa c ni pamoja na maendeleo ikiwapo hizi ofisi?Nawasilisha kutoka Mwanza