Mapambano Yetu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,124
- 2,092
suala la mtu mmoja kuvamia mkutano au kundi la watu tena mchana kweupe na akakosekana wa kupata sura yake wakati kundi kubwa la waandishi wa habari lipo na linachukua picha + kurekodi matukio ni uzembe wa hali ya juu sana. Kumbe Jambazi anaweza kutumia mwanya huo tena mbele ya vidume na kutekeleza mauaji still asiwepo wa kutoa sura yake. Huu ni woga wa hali ya juu kwa watanzania. Hivi kweli alikosekana angalau shujaa mmoja wa kumvua kofia tukamfahamu? Kwa woga wetu tunatoa nafasi kwa vyombo vya usalama kukana maovu yao. Wengi wetu tunaamini kuwa matukio ya aina hiyo hutekelezwa na vikosi maalumu kutoka kwenye majeshi Yetu, lakini hayupo wa kurithibitisha hilo kwa sababu sisi ni waoga.
Mara nyingi vikosi vya ulinzi na usalama vimekuwa vikiyakana mashtaka ya aina hii kuwa hawahusiki. sasa Naomba IGP atangaze rasmi kuwa ni marufuku kwa askari wake kwenda kumkamata au kumshurutisha yeyote akiwa ameficha sura yake ilhali hayuko kwenye mavazi ya kijeshi (kiaskari). Na sisi wanajamii tuelimishwe kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayefanya hivyo. Ipo siku tutakuja kujilaumu kwa kufanya makosa ya ajabu kama haya. wenzetu wanatumia technologia kuwatafuta wanaofanya uhalifu mafichoni. Sisi watanzania tunataka zitumike kamera za CCTV hata kwenye matukio ya wazi tena mbele ya waandishi wa habari.
Si Amiri Jeshi Mkuu, CDF wala IGP aliyewahi kujitokeza na kukemea tabia za watu kutumika Kama Jeshi huku wakiwa wameficha nyuso zao. Hii ndio inatufanya tuliowengi tuamini kuwa hao vijana mnawatuma nyinyi. Watanzania, Hili ni tatizo tena kubwa sana. Tuungane kutokomeza tabia hii. Nawasilisha
Update
Mwigulu: Aliyemtishia bastola Nape sio Polisi