sinafungu
JF-Expert Member
- Feb 13, 2010
- 1,527
- 865
Mbarali ilivyokwepa wazabuni kuokoa milioni 800 kutengeneza madawati;
Tathmini iliyofanywa na wataalamu wa halmashauri ikabainisha kuwa shule za wilayani humo zina madawati 12,889 tu huku mahitaji yakiwa ni madawati 18,860.Hii ikimaanisha kuna upungufu wa madawati 5,971.
Ndipo likaja wazo la halmashauri kuwa na karakana yake ili kutengeneza madawati hayo hali ambayo si tu kuwa itapunguza gharama za kutengeneza madawati hayo bali pia kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana wenye ujuzi wa useremala wilayani hapo.
Mkakati huo utaiwezesha halmashauri hiyo kupunguza matumizi ya fedha za madawati hadi kufikia Sh milioni 235 kutoka milioni 800 ambazo ingetumia kama ingechukua wazabuni.