Egwugu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,558
- 8,556
Ni siku zimepita kidogo tokea watoto wale wapotee katika ajari yya kutisha kweli kweli. Mungu awatangulie na azilaze roho zao mahala pema peponi, Amina.
Pamoja na haya yoote yaliyotokea na yanayoendelea, bado kuna mambo yananichanganya sana. Kuna hili suala la Nyalandu kuingilia kati ishu hii. Kuna hili la serikali kuonekana wanahusika na tukio mapema huku wakitegea kuzipiga rambirambi kama zile za tetemeko Kagera. Kuna hii spidi ya watu kuonekana kila mmoja anataka asikike kupitia tukio hilo.
Haya mambo yakoje haswa? Nani ni nani na kipi ni kipi haswa? Swali langu kuu na la msingi.
Ya Arusha tumeyaona, nauliza: Hivi haya yote ni kutokana na kwa vile waliokufa ni watoto? watoto waliokufa ni wengi sana? Msiba kweli ni mkubwa sana? Kwasababu waliokufa wanatokea Arusha? Kwasababu ni shule kubwa yenye jina? Ama ni kwasababu wale ni watanzania wenzetu na tunahusika kwasababu ni watanzania wenzetu?
Naomba tujiulize tena: Hivi siku moja kilichotokea Arusha kikatokea kesho kwingineko Mfano Kyamulaile, Koromije, Ikwiriri, Kazolamimba, Nyanguge, Kakonko, Iyombakuzova, n.k, ni kweli hawa nao watatetewa, kusaidiwa na kuchukuliwa kama hawa wa Arusha? Sisi kama watanzania tutakuwa tayari kulia pamoja kama tulivyolia kwa hawa wa Arusha? Hatutajari wanatokea wapi na ni wa shule gani?