Hili la supermarket limekaaje

Kyodowe

JF-Expert Member
Mar 6, 2013
922
1,000
Kwanza nieleweke kama kawaida wikiendi huwa napenda kufanya shopping kwa ajili ya kukimbiza ka-wiki. Cha kushangaza toka imeanza awamu hii ya5 kila ninapokuwa nimefanya manunuzi kwenye hizi supermarket zetu lazima niambulie kabidhaa kamoja fake/expired.

Nimekuwa najitahidi kuhama hama kwenye hizi supermarket kila ninapoona sipati huduma bora lakini matokeo yanakuwa ni yaleyale.

Je, hivi hizi ni dalili za kuporomoka kiuchumi? Au ni nini hiki kinachoendelea mpaka masurpermarket zinakuwa ni vitu vilivyooza!

Angalizo kwa wale mnaopenda thread za makinikia tuvumiliane kidogo ili tuweze kujuzana hili.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
39,645
2,000
Hebu weka wazi ni supermarket gani hio ili uokoe wengine. Isije kuwa duka kubwa la mchagga/mpemba unaita supermarket.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,660
2,000
Nitahamia huko mkuu
Tanzania ni nchi ambayo watu wengi wanaishi kwa ujanja ujanja. Si hosptalini (ukizubaa unachomwa sindano iliyo expire), Si mtaani, si nyumbani. Cha muhimu ni kuwa makini tu kwani ndio njia ambayo watanzania tumeamua kuifuata na haina uhusiano wowote na hali ya uchumi wetu. Labda nikushauri tu. Kwa Tanzania kuna bidhaa nyingi sana unazoweza kuzipata mitaani bila kwenda huko supermarket. Tena unapata zipo katika hali ya nzuri zaidi. Mboga? Unga wa mahindi? Mchele? Matunda? Juice? Vyote hivi vipo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom