Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Jul 22, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Na Privatus Karugendo

  KATIKA vyombo vya habari, jana tumesikia CHADEMA wamegundua mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu na hasa ujumbe mfupi wa maneno. Na kwamba mtambo huu umeingizwa nchini kutoka Israel na mtoto wa kiongozi wa CCM; na kwamba mtambo huu umetumika tayari kuingilia mawasiliano ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA, kwenda kwa baadhi ya viongozi wa CCM kwa lengo la kuwatishia maisha.

  Ujumbe unaonekana umetoka kwenye simu za viongozi wa CHADEMA, lakini ukweli ni kwamba ujumbe unakuwa umetengenezwa na mtambo ulionunuliwa Israel na kuupitisha kwenye mtandao wa simu za viongozi wa CHADEMA. Na kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tayari ametangaza nia ya kuwafikisha viongozi wa CHADEMA mahakamani kwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwenye simuzao uliokuwa unawatishia maisha baadhi ya wanachama wa CCM.

  Sikushangazwa na habari hizi na wala sina mashaka kwamba kitu hiki hakiwezekani. Tumeshuhudia "majambazi" wa mtandao wanavyoingilia mtandao wa barua pepe; mtu anaingilia anwani yako na kuwatumia marafiki zako ujumbe kwamba umetekwa, au umeibiwa ukiwa nje ya nchi na unahitaji msaada wa fedha. Hili limewatokea watu wengi. Pia tunajua jinsi watu hawa wabaya wanavyoweza kutuma virusi kwenye kompyuta na wakati mwingine kutumia teknolojia kuiba habari nyeti kutoka kwenye kompyuta za watu; pia tunasikia kila siku jinsi "majambazi" hawa wa mtandao wanavyoingilia akaunti za watu kwenye benki na kuiba fedha. Hivyo na hili la kuingilia ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu za watu linawezekana kabisa.

  Hoja yangu ni kwamba CHADEMA, wamefanya haraka kutangaza jambo hili. Wangefanya subira na kuhakikisha wanamnasa mtu huyu na mtambo wake. Kutangaza kabla ya kumkatamata ni hatari! Wao wametangaza mtu huyu ana fedha nyingi na kwamba ni mtoto wa mtu mkubwa. Hivyo uwezekano wa kuhakikisha mtambo huu unaangamizwa na kupoteza ushahidi ni mkubwa; au mtambo huu kwa miujiza ukageuzwa kuwa ni mali ya CHADEMA ni kitu cha kawaida kabisa; kama Jambazi anaweza kuingia kanisani na kuungama dhambi ya kumteka mtu na kumtesa; Jambazi huyo akakamatwa bila kuonyeshwa sura yake na kufikishwa mahakamani kimya kimya na kutumia tukio hilo kuzima mjadala mzima wa tukio hilo la kinyama la kuteka mtu na kumtesa
  kwa kisingizio cha kesi kuwa mahakamani, kila kitu kinawezekana! Pia, uwezo wa fedha kuingilia uchunguzi wa suala zima la mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu kwa kuziba midomo na akili za wataalamu wa teknolojia nchini ni mkubwa sana. Kwa vile kumekuwepo na shutuma hizi za kutumia teknolojia vibaya kwa muda mrefu, sasa ulikuwa ni wakati muafaka wa kuwakamata watu hawa na kuwafikisha mbele ya sheria.

  Uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ilisikika pia kwamba mtoto wa kiongozi mkubwa alifanya mpango kwa kuwaleta wataalamu wa data na kuhakikisha kura za urais zinavurugwa. Jambo hili lilisikika sana kwenye vyombo vya habari, kufikia hata kutaja sehemu iliyotumika, kompyuta zilizotumika na programu zilizotumika, lakini hakukuwepo na ufuatiliaji. Hili ndilo kosa kubwa tunalolifanya hapa Tanzani. Mambo yanajitokeza na wakati mwingine ni mambo ya uhakika kabisa, lakini ushahidi mzito unakosekana.Tunabaki kwenye maneno mengi na porojo. Huku wenye nia mbaya na uchu wa madaraka wakiendelea kusonga mbele kwa kasi ya kutisha.

  Tumesikia jinsi watu walivyotumia teknolojia na kujitengenezea Luku na kuziuza kinyume na mfumo wa TANESCO. Watu hawa watakuwa wamejitengenezea fedha nyingi wakati TANESCO inaingia kwenye hasara kubwa hadi kufikia hatua za taifa kuingia gizani. Na fedha hizi wanazozitafuta kwa mbinu chafu, inawezekana ni kwa lengo zima la kutafuta madaraka 2015. Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna wajanja wanaotengeneza kadi za muda wa maongezi wa kampuni mbalimbali za simu, na kuwauzia watu.

  Ninachoaamini ni kwamba wezi wa kutumia teknolojia ni lazima kuwakamata kwa kutumia teknolojia kama ulivyo msemo wa Kiswahili wa dawa ya moto ni moto. Na hapana shaka kwamba mtu akitumia ujumbe mfupi wa maneno kwenda kwa mtu ni lazima mtu huyu atambuliwe.

  Pamoja na mchakato mzima kwa kuzisajili simu zote; ni lazima mitambo ya makampuni ya simu ya kurushia ujumbe huu mfupi itakuwa na uwezo wa kutunza ujumbe huu na kuweza kutambua unatoka kwenye simu ipi, yenye uwezo upi na iliyotengenezwa na kampuni ipi na mwaka upi. Na kama ujumbe umeingiliwa namtambo mwingine ni lazima mitambo ya makampuni ijue. Na ikitokea ni ukweli kwamba mtambo huu wa kuingilia mawasiliano ya simu upo hapa Tanzania na makampuni ya simu hayajui, basi ni lazima tuwe na mashaka na makampuni haya. Vyovyote vile ni lazima makampuni haya yawajibishwe; kama si kwa kushirikiana na "majambazi" wa mtandao basi yawajibishwe kwa uzembe! Haiwezekani mtambo mwingine uingilie mfumo wao wa mawasiliano na wao wasijue. Kama hili la CHADEMA ni la kweli, basi makampuni ya simu yatakuwa yanafanya kazikwa makubaliano na "Majambazi" wa mtandao.

  ADDITION:
  Tatizo letu hapa Tanzania ni kwamba tunaingiza siasa kwenye mambo yote. Biashara na uwekezaji tumeingiza siasa. Baadhi ya wanasiasa wana hisa kwenye makampuni mbalimbali yanayowekeza kwenye taifa letu. Habari za kuaminika ni kwamba hata makampuni haya ya simu kuna wanasiasa ambao wana hisa kule. Kama hili ni kweli, basi uchunguzi wowote juu ya mawasiliano ya simu (na kama uchunguzi huo unawagusa wanasiasa) ni vigumu kufanikiwa.

  Katika hali ya kwaida, si suala gumu kufuatilia na kujua ni nani amempigia simu nani, siku gani na kwa muda upi, au kufuatilia na kugundua ni mtu gani ametuma ujumbe mfupi kwa nani na kwa wakati gani. Pia si suala gumu kufuatilia na kujua kama haya makampuni ya simu yanatuibia kwa kubinya uwiano wa malipo na muda wa maongezi. Kwa maana kwamba mtu anapolipa elfu moja anaongea kwa muda wenye thamani ya elfu moja. Wanaweza kutoa ofa ya kuongea bure kwa kipindi fulani, au kutoa zawadi mbalimbali, lakini huku wakijua jinsi watakavyotukamua kwenye muda wa maongezi. Hivyo CHADEMA, wangeenda pole pole, kwa uhakika na kwa uchunguzi wa kina, wangeweza kugundua mengi juu ya mfumo mzima wa mawasiliano ya simu. Nao wangeenda Israeli, na kutengeneza mtambo wa kukamata mitambo inayoingilia mawasiliano. Tena wangeenda kwenye kampuni hiyohiyo iliyotengeza mtambo huo wa kuingilia
  mawasiliano ya ujumbe mfupi. Huo ndiyo mchezo wa makampuni makubwa katika mchakato mzima wa ubeberu na unyonyaji. Wanatengeneza virusi vya kushambulia mtandao, na wakati huohuo wanatengeneza silaha za kupambana na virusi hivyo. Kwa njia hii wao wanatengeneza faida kubwa kwa maumivu ya watu wengine.

  Taifa letu sasa hivi linapita katika kipindi kigumu sana. Na kufikia uchaguzi mkuu wa 2015, tutashuhudia mengi. Hivyo ni muhimu CHADEMA na watu wengine wenye nia njema na taifa letu kuvuta subira kwa matukio mbalimbali, ili tuweze kuwafichua majambazi na watu wenye nia mbaya na taifa letu. Mfano hili la kuingilia mawasiliano na kuwachonganisha watu kiasi cha kufikishana mahakamani ni kitendo kibaya kiasi kwamba kinaweza kutufikisha katika umwagaji damu.

  Tutapambana na watu hawa wabaya kwa kupiga hatua za uhakika; na hatua muhimu ni kuwakamata watu hawa wakiwa kazini. Kuwakamata kwenye mazingira ambayo hawawezi kwa namna yoyote ile kukwepa na kuweza kutunga hadithi kama ile ya mtuhumiwa kwenda kutubu Kanisani.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  ADDITION:
  Tatizo letu hapa Tanzania ni kwamba tunaingiza
  siasa kwenye mambo yote. Biashara na
  uwekezaji tumeingiza siasa. Baadhi ya
  wanasiasa wana hisa kwenye makampuni
  mbalimbali yanayowekeza kwenye taifa letu.
  Habari za kuaminika ni kwamba hata
  makampuni haya ya simu kuna wanasiasa
  ambao wana hisa kule. Kama hili ni kweli, basi
  uchunguzi wowote juu ya mawasiliano ya simu
  (na kama uchunguzi huo unawagusa wanasiasa)
  ni vigumu kufanikiwa.
  Katika hali ya kwaida, si suala gumu kufuatilia
  na kujua ni nani amempigia simu nani, siku
  gani na kwa muda upi, au kufuatilia na
  kugundua ni mtu gani ametuma ujumbe mfupi
  kwa nani na kwa wakati gani. Pia si suala gumu
  kufuatilia na kujua kama haya makampuni ya
  simu yanatuibia kwa kubinya uwiano wa malipo
  na muda wa maongezi. Kwa maana kwamba
  mtu anapolipa elfu moja anaongea kwa muda
  wenye thamani ya elfu moja. Wanaweza kutoa
  ofa ya kuongea bure kwa kipindi fulani, au kutoa
  zawadi mbalimbali, lakini huku wakijua jinsi
  watakavyotukamua kwenye muda wa maongezi.
  Hivyo CHADEMA, wangeenda pole pole, kwa
  uhakika na kwa uchunguzi wa kina, wangeweza
  kugundua mengi juu ya mfumo mzima wa
  mawasiliano ya simu. Nao wangeenda Israeli,
  na kutengeneza mtambo wa kukamata
  mitambo inayoingilia mawasiliano. Tena
  wangeenda kwenye kampuni hiyohiyo
  iliyotengeza mtambo huo wa kuingilia
  mawasiliano ya ujumbe mfupi. Huo ndiyo
  mchezo wa makampuni makubwa katika
  mchakato mzima wa ubeberu na unyonyaji.
  Wanatengeneza virusi vya kushambulia
  mtandao, na wakati huohuo wanatengeneza
  silaha za kupambana na virusi hivyo. Kwa njia
  hii wao wanatengeneza faida kubwa kwa
  maumivu ya watu wengine.
  Taifa letu sasa hivi linapita katika kipindi
  kigumu sana. Na kufikia uchaguzi mkuu wa
  2015, tutashuhudia mengi. Hivyo ni muhimu
  CHADEMA na watu wengine wenye nia njema
  na taifa letu kuvuta subira kwa matukio
  mbalimbali, ili tuweze kuwafichua majambazi
  na watu wenye nia mbaya na taifa letu. Mfano
  hili la kuingilia mawasiliano na
  kuwachonganisha watu kiasi cha kufikishana
  mahakamani ni kitendo kibaya kiasi kwamba
  kinaweza kutufikisha katika umwagaji damu.
  Tutapambana na watu hawa wabaya kwa kupiga
  hatua za uhakika; na hatua muhimu ni
  kuwakamata watu hawa wakiwa kazini.
  Kuwakamata kwenye mazingira ambayo
  hawawezi kwa namna yoyote ile kukwepa na
  kuweza kutunga hadithi kama ile ya
  mtuhumiwa kwenda kutubu Kanisani.
   
 3. m

  markj JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  wa israel wanachangia kutokomeza amani ya hii dunia kama ni kweli, kwanini watengeneze kitu kama hiki ambacho hakina manufaa yoyote yale kwa upande wowote zaidi ya kuchochea ugomvi! inamaana ntu kama mmarekani anaweza kureceive mawasiliano white house yakiwa kama yametumwa na ikulu ya urusi1 kumbe sio,wamejitumia wao kwa kutumumia aina ya kifaa kama hiki! na vitakuwa viko more advanced tena waweza kuta kikawachapiga hata simu sasa na si sms! :shetani:
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ccm ni kama mtu anayekata roho...maana wanahangaika kweli..huyo werema ndo mbumbumbu kabisa hata sijui aliupataje huo uanasheria wa serikali
   
 5. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  [Samahani wakuu, nilikuwa nasaidia ku-edit
  maana mimi binafsi ilikuwa inanitia uvivu kuisoma
  ]

  Nyetk
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mraji and Ridhiwani at work. Shida ya kuendesha kamoeni kifamilia unakuta hata majukumu ya kirais familia nayo inadhani inawajibu wa kuyatekeleza pia!
   
 7. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu Nyetk, maana kimchina changu kilishapata moto!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ukiwa umejifungia kwenye box ndiyo unaweza kuona tecknology ya aina hiyo haina maana yeyote. Lakini kwa Isreal inaweza kuwa na maana sana hasa kwenye masula ya UJASUSI.

  If your memory still serves you well, kumbuka Waisrael walipoingilia mawasiliano ya IKULU ya Uganda enzi za Idd Amin na kwenda kuwakomboa mateka wao walikuwa wamtekwa na kuondoa Entebbe, bila Amini kufahamu.

  Scenerio nyingine, kwa wale tuliokuwa Arusha wakati wa ujio wa Rais Clinton (Sio Bush) wa USA. mawasiliano yote ya simu, internet etc yaliingiliwa na FBI/CIA(?) Arusha nzima ikawa haina mawasiliano kwa masaa kadhaa. Kwa wamarekani walifanya hivyo kwa sababu ya usalaama.
   
 9. wizaga

  wizaga Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana kabisa na maneno yako,technogia hizi zipo duniani mfano vita vya waamerika nchini iraqu vyombo vyao vya mawasiliano kutoka iraq kwenda amerika vilikuwa vinaingiliwa na vifaa vya mawasiliano toka urusi lakini wenzetu wajanja waligundua mapema na kutumia tech nyingine pia osama bin laden alikuwa anauwezo wa kuingia kwenye sore au server za white house na kujua walichopanga lakini obama alipoingia madarakani akachenge to victory
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  naona justification zote za matumizi ya hii technologia yamejikita kwenye misingi ya kivita. kwani na sisi tuko vitani?
   
 11. H

  Haki Yetu Senior Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mtoa mada nadhani umesahau kidogo, hivi unakumbuka issue ya mkuu wa wilaya Igunga ilivyokua? Unajua hukumu yake imekuaje?

  Unakumbuka sakata la kukamatwa kwa lori lililojaa masanduku yenye kura jijini Mbeya? Mwisho wake nalo ulikuaje?

  Hilo la hao vijana wa mkuu waliowaleta wenzao kuvuruga kura za urais kwa teknolojia, kwani si hadi mahali wanapofanyia shughuli yao palitajwa, nalo lilikwisha vipi?

  Kutokana na hayo yote walivyosema mapema yote ni sawa kabisa mkuu, utakapomkamata na mtambo huo utashangaa polisi ndo wanaukimbiza na kuuficha na kesi inakurudia wewe!
   
Loading...