barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Wakati mwingine ukikaa na kutazama "siasa" za Afrika na hususani Tanzania kama nchi mama,unapata kigugumizi cha fikra na aina ya maisha ambayo sisi kama wa Waafrika na Taifa kwa ujumla tunayaishi.
Wanayoyaongea wanasiasa sio yale wanayatenda.Unaweza kuwa unamuheshimu sana Rais,Mbunge au diwani,lkn ukitazama matendo yake na nia juu ya wananchi wake unabaki "kumdharau" sana.Hata kama ni dharau za nyuma ya keyboard ili kunusuru uhai wako,lkn bado uamdharau tu.
Kuwa na siasa za upinzani(vyama vingi) katika Afrika ni unafiki sana.Na sijui hawa watu huyo Mungu wao wanaomwabudu huwa wanamwambia nini wawapo katika usiri wa kiroho.
Mwaka 2010,kwenye jimbo la Maswa Mashariki,mgombea wa CCM wakati huo,ndugu Simon Kisena ambaye ndiye mmiliki wa UDA na UDART.Mgombea huyo alimpiga "ngwara" Kamanda wa Wilaya.Afande alikula ngwara mbele za watu na vijana wake.Kisena ndio huyo anadunda na UDA ya magumashi na UDART yenye usanii.
Usiongelee juu ya Job Ndugai na Chilongani.Na ili kumpoza bwana Chilongani,basi mamlaka zikampa Ukuu wa Wilaya ili asahau kipigo cha fimbo ya kichwa.
Kali ya mwaka ni ile ya Dr Titus Kamani,wakati huo akiwa mbunge na Waziri wa Mifugo,huyu kila mahali alionekana akiwafanyia fujo watangaza matokeo na kuwasukuma polisi huku na kule.Hili nalo lilipita.
Watawala wanataka kutuaminisha kuwa kuna kundi linaloweza kuadhibiwa likivunja sheria na lingine hapana.
Ndio maana Selukamba alivyotamka fu*** bungeni aliendelea kudunda tu.Haya yote watu wanayanukuu na kuacha yapite kwa muda,ila siku wakichoka watayafukunyua.
Haki huinua Taifa.