Hili la kuitana "Mtoto" au "Mbwa Mwitu" ni kukosa Busara ya Uongozi !

Hashim bin Faustin

Senior Member
Jan 30, 2017
177
216
Nimesikitika sana kusikia viongozi wa kitaifa wakitumia misemo ya "Wewe Mtoto/Kelele za Mbwa Mwitu" katika kujibu hoja zinazo muandama. Je hii ni busara ?? Wakati taifa liko kwenye fukuto kubwa la kuhatarisha amani ya taifa letu tunakutana na viongozi wasiokuwa na busara hata kidogo katika kusimamia utendaji wao wa kila siku kufikia kuwa na kauli za kuudhi/kudhalilisha/kubedha wengine hii haikubaliki hata kidogo.

Inaonyesha ni vipi kama Taifa tunakosa Vijana waliopikwa na kupikika katika suala zima la uongozi kwa ujumla wake. Kama wananchi waelewa tunabidi kwa nguvu zetu kwa pamoja tuanze kukemea hii hali ili viongozi hawa wajuwe tunawaona na kusikia ujinga wao wanao ufanya. Tunahitaji vingozi makini wenye Busara na Wenye nia ya Kweli katika kutumikia Taifa letu kwa kusimamia Haki ya Kila Mtanzania bila Kuvunja sheria za Nchi yetu wenye Kuilinda na Kiitetea Katiba yetu ya Tanzania bila Upendeleo wowote na Bila woga na unafiki kwa kupandikiza chuki kwa watu wengine na kuwachafua eti kudhibitiana kiongozi !!

Pia tunalaani vikali kitendo chochote cha kuchafuana kisiasa kwa faida fulani ya kundi fulani. Wote ni Watanzania lazima tupendane na kutendeana Haki. Wote tunahitaji kufaidi Keki ya nchi hii kwa Usawa bila upendeleo wowote. Ukiwa ccm / chadema/cuf nk. Wote ni Watanzania na tuna Haki sawa.

Viongozi wa Serikali lazima muwe makini katika hili , hasa Viongozi Vijana , kwani Vijana lazima muwe na tahadhari katika kutimiza majukumu yenu ya kila siku kwani safari bado ndefu msije mkajitia Kilema wakati hamjamaliza kuvuka Mito na Mabonde mbele ya Safari yenu. Busara ya kweli ! Kumuogopa Mungu ki kweli na Kutenda Haki ndiyo salama yenu katika kufanikisha ndoto zenu , .Lasivyo mtasindikiza wazee walio tangulia na nyie kuishia njiani kwa kukubali kutumika ovyo ovyo tu !

Nawasilisha....!!
 
Hayo maneno uliyoyakariri, yametumiwa na kiongozi gani? Kwasababu sijawahi kumsikia kiongozi yeyote jatamka hayo.
 
Kuna mdau alisema viongozi wetu wanahitajika kupelekwa tena ngurudoto wakapewe semina elekezi
 
Ila kusema watu ni "wapumbavu na malofa" ni kauli ya busara sana

Mwafwaa ni neno la hekima sana kutumika kwenye maafa.

Anyway kama unasikia njaa si ukapike ule? Au unataka nikakupikie??
Yote yanahusika na ni ya kukemea !
 
Back
Top Bottom