Hili la Ethiopia kupitishia mizigo yake bandari ya Dar es salaam limekaaje?

Se-ronga

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
650
909
Nawasalimu wana JF.!

Nchi yetu imeendelea kupokea ugeni wa viongozi toka mataifa jirani na hata nje ys bara letu la Afrika,wengi wa waliofika wameonyesha nia thabiti ya kujenga/ kuendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri na nchi yetu hasa kwa suala zima biashara na uchumi

Juzi tumepokea ugeni mwingine wa Waziri Mkuu wa Ethiopia ambaye pamoja na mambo mengine inasemekana kuna mikataba imesainiwa kati ya Tanzania na Ethiopia kwa ajili kuimarisha ushirikiano hasa eneo usafirishaji,elimu na biashara

Binafsi nafurahishwa na ushirikiano huu,ikizingatiwa kwamba Ethiopia ni moja ya nchi katika bara la Afrika ambayo taarifa na takwimu za Benki ya Dunia zimeonyesha uchumi wake unakua kwa kiwango kizuri

Suala ambalo sijalielewa kuhusiana na ujio wa ugeni huu ni hili la "ETHIOPIA KUPITISHIA MIZIGO YAKE KWENYE BANDARI YA DAR ES SALAAM".Ninachofahamu ni kwamba kwa sasa mizigo mingi ya nchi hii inapitia bandari ya Mombasa-Kenya pamoja na Djibouti.Na ili kurahisisha usafirishaji kati ya Kenya na Ethiopia kuna barabara ya lami imejengwa kuunganisha mpaka wa nchi hizi (nafikiri imeshakamilika)

Taarifa nilizosikia na kuona kupitia vyombo mbalimbali vya habari ni kwamba Taifa hili kubwa la pembe ya Afrika lenye wakazi zaidi ya mil.80 litaanza kupitishia mizigo ya kutoka na kuingia nchini kwake kwa kutumia bandari yetu ya Dar es salaam

Kila nikitafakari kuhusiana na hili suala la mizigo ya Ethiopia kupitia bandari ya Dar es salaam naona kama kuna ugumu hasa kwa kuzingatia umbali uliopo kati ya Addis na Dar es salaam ukilinganisha na bandari za Lamu, Mombasa na Djibouti.Au kuna sababu zingine ambazo kwa sisi tunaolitazama kwa macho mawili hatuwezi kuziona

Kwa wale wenye uwezo wa kuliona hili kwa jicho la tatu hebu tupeni ukweli wa mambo juu ya hili suala la mizigo ya Ethiopia kupitishia mizigo yake bandari ya Dar es salaam
 
Naomba kuuliza haya makubaliano baina ya nchi na nchi,je kama nchi moja imeenda tofauti wanaweza kushtakiana?
 
Back
Top Bottom