Hili jambo lilinisumbua sana

Hili jambo lilinisumbua sana

affinitytz

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2020
Posts
234
Reaction score
1,043
Miaka kadhaa nyuma, nilikutana na binti pale Euro H survey sijui panaitwaje siku hizi.
Nikamuelewe binti, nikaomba namba akakataa.
Siku mbili baadaye nikiwa nakula chakula cha usiku binti akaja tena. Kwa ajabu akaja akaa kwenye meza niliyokuwa nimekaa. Tukisalimiana na alipomaliza kula akaniachia namba bila kumuomba. Miezi minne baadaye tukawa wapenzi.
Baada ya mwaka, nikiwa nimehudhuria kikao cha harusi ya familia nikashangazwa na binti naye amehudhuria. Katika utambulisho ndio nikagundua kuwa ni mtoto wa mmoja wa mama zangu wadogo upande wa mama. Mama yangu na mama yake ni watoto wa mama mdogo na mama mkubwa.
Nilirudi kwangu nikiwa na huzuni sana maana tukipanga kuoana. Hii ilibaki kuwa siri yetu.
Mahusiano hayakuisha haraka, tuliendelea kubanjuana mpaka siku tulipoamua kuacha.
Ameolewa na nimeoa. Namheshimu kama dada.
 
Ilimtokea jamaa yangu Mzumbe University alimwelewa binti wa mwaka wa kwanza wakaanzisha mahusiano.
Baada ya miezi kadhaa baba wa binti amekuja kumtembelea mtoto wake akakutana na jamaa na kumwambia "mdogo wako yupo hapa", kuja kutambulishwa kumbe ni yule binti.....

Ilibidi tukae kikao cha dharura ila msela aliendelea kujilia vyake. Sijui wanaendeleaje huko walipo.
 
Inamaana hawakujuana ilihali Ni ndugu baba mmoja?? Au mmoja alikuwa mtoto wa pembeni
 
Back
Top Bottom