HIVI NJAA YAWEZA FANYIWA UTANI SIKU HIZI? AU NI KEJELI ZA WALIOSHIBA?
Kumekuwepo na tetesi hapo nchini kwetu za kuwepo kwa janga la njaa, jambo ambalo limekanushwa kwa kauli kali na Rais wetu katika mkutano wake pale Bariadi. Pamoja na kwamba tuko nje ya nchi yetu lakini tunaona si jambo jema kukanusha ukweli wa tukio kubwa kama hilo, hususani kama limesha anza kujitokeza au kuwepo kwa dalili za njaa. Ni wazi tunao ndugu, jamaa na marafiki pia ambao wameanza kutupigia yowe la kuomba msaada kwa hali ilivyo sasa nchini kwetu. Naomba siasa iwekwe pembeni kwanza, taarifa sahihi zikusanywe kwa haraka kupitia vyanzo vya serikali tujue ukubwa wa tatizo na huduma ya dharura ianze kutolewa kwa wahanga. Maneno hayana tija Ikulu ya Dar es salaamu inaongea mno sasa tunahitaji utekelezaji wa haraka katika hili.
Wanao mshauri Rais waache kumpotosha kwa sababu ya hofu ya kulinda vyeo na madaraka yao, itakuwa aibu kubwa kwa taifa linalojinasibu usiku na mchana kuwa uchumi wake umepanda wakti wananchi wana lala njaa na maisha ni duni. Nawasihi Mawaziri na viongozi waandamizi waache kumwogopa Rais. Rais ni raia tu tuliye mpa heshima na madaraka ya kutuongoza, ana haki zake kikatiba kwa sababu ya demokrasia hiyo, lakini Wananchi kama waajiri wake wa mwisho tuna haki ya msingi ya kumwonya na kumrekebisha na asipokuwa msikivu tuna haki ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake. Na hayo ndiyo mamlaka ya kikatiba ya wananchi yanayo tajwa na katiba yetu. Kwa hiyo suala la njaa siyo jambo la ku compromise, Rais isikemee tu na ijiridhishe kwa kufika na kuona kwa macho yake huko kunako tajwa kuwepo kwa matukio ya njaa na huo ndio utumishi tunao uona hapa ughaibuni. wenzetu hapa janga dogo tulikitokea utaona breaking news na wakuu wote wa serikali wako pale kutafuta suluhu mpaka tatizo liishe.
Mwisho ni shauri serikali yetu iwekeze kwa kiwango kikubwa sasa katika kilimo cha umwagiliaji kupitia ziwa Victoria, lukwa, tanganyika, nyasa na mito mikubwa. kuna mahitaji makubwa mno ya chakula duniani kuliko wakati wowote na ni biashara ya uhakika zaidi kuliko kukimbilia hivyo viwanda tunavyodhani. Kwa ujumla mapinduzi ya viwanda yanaanza na uwekeaji mpana katika elimu, elimu na elimu maana yake ni rasilimali watu wenye ujuzi wa kubadili rasilimali ghafi kuwa bidhaa mbali mbali. Pili mitaji, tatu miundo mbinu na mwasiliano, nne masoko, tano sera na sheria n.k.
Kama mikoa inayozunguka maziwa nilo taja ingekuwa na scheme kubwa za kilimo cha umwagiliajia na Bonde la Morogoro likafanyiwa kazi vizuri tungeaga umasikini haraka sana
Kuna upungufu wa zaidi ya asilimia 47% ya chakula duniani sasa, hata hapo jirani kenya wana hitaji chakula, sudan, ethiopia, eritrea, somalia,chad,afghanstan, iraq, lebano, syria n.k yaani kweli hatuoni soko hilo lisilo na mashariti?
Asanteni wana jamvi
UFO-Ughaibuni