Hiki ndicho Kinafanya Tanzania Iwe Na Amani!

KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,822
2,290
Unajua Tanzania Ingekuwa Nchi nyingine basi Mda huu tungekuwa Tunasikiliza milio ya mitutu kama miziki na huku tukishuhudia samu za watu kila kona kama machinga pale stand ya k/koo.
Hakuna Kiongozi Atakayejisifu Kuwa Anasimamia Amani Tanzania ama Kaiweka Amani Tanzania.
NARUDIA TENA HAKUNA KIONGOZI ANAYEPASWA KUJISIFU KUWA ANASIMAMIA AMANI TANZANIA.
Maana viongozi wao ndio wanakuwa wakwanza kuvunja amani kwa namna ya Uongozi wao
Tumshukuru Mungu Kwa kuweka Tanzania Ya Wakristo Walioshika Dini Na Waisilamu Walioshika Dini.
Tukiona Serikali Inavyotuzungusha Yaani Tukiwaza vitabu Vyetu Vitakatifu Basi Tunafumba Macho Na Kuvumilia Yote.
Kiongozi Wewe Unayesema Unasimamia Amani TANZANIA nakuambia KWeli Watanzania TUna Hofu Ya MUngu Ndio Maana Tunatulia Ila Hauna Hata Chembe Ya Kusimamia Amani.
Kuamua Kufa Kwa Ajili Ya Nchi Yetu Inawezekana Kabisa Ila Tunawaza Mungu Anatuusi Tuishi Kwa Amani.
Watanzaia Wenzangu Na Tuzidi Kushika Dini Zetu Ili Tuitunze Amani Yetu Zaidi Na Zaidi, Amani Yetu NI Sisi WEnyewe Tulio Nayo Wala Sio Kiongozi Yeyote maana Tukiasema Tutakufa Kwa Ajili Ya Nchi Yetu. Hata Kwa Mitutu Ya Bunduki Hakuna Wa Kutusimamisha.
Viongozi Wanatupoteza sisi wenyewe na hawajui damu za watu wasio na hatia zinatutia kichefu chefu NA Hawajui Zinaweza Kututapisha Na Wajifanya Wansimamia Amani.

Kwakweli Amani Tunayo Sisi Wenyewe Wananchi Kwakuwa Tunahofu Ya MUNGU Na WAla Hatuna hofu ya Kiongozi Hata Akiwa anatuchinja usiku kama kuku wake waliobandani.

Amani Yetu Tanzania Tunayo Sisi Wenyewe Wananchi Tuzidi Kumcha Mungu Kwa Dini Zetu Zote Ili TUzidi Kudumu Katika Amani Yetu.

AMANI YA TANZANIA INASIMAMIWA NA WATANZNIA WENYWE NA WALA SI KIONGOZI

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE NA UWASAMEHE VIONGOZI WANAOONA SISI WATANZANIA NI SAWA NI KUKU ZAO TENA ZILE BLOILER
 
Mkuu, msumari wako wa moto sana!!
Mwenyewe huwa anasema... "msg sent and delivered"..
Hakika msg imewafikia.

HATUENDI KWA SWAGA ZA KUCHAPWA NA KUBEMBELEZWA NAPIPI KAMA MTOTO MDOGO
UKWELI WAUJUE SIO WANAJITAPA WANAFANYA WAKATI MAMLAKA YENYE MABAVU TUKIAMUA WANACHI KUIPINGA NI VITA.
SASA WAJUE HATUTAKI SIO TUNAOGOPA SISI TUNAMUANGALIA MUNGU WETU KWA KWELI
 
Inawezekana unaiweka Tanzania katika mzani wa familia yako!

Hayo mabaraza ya wazee yako wapi? Kwani wao sio viongozi? Au neno uongozi unalielewaje?

naelewa ni mtu anayechinja watanzania wanaoongea ukweli na kuzuia vyombo vya habari vinavyotoa habari za ukweli na kutaka kila mtu amtukuze yeye hata kama anakosea hiyo ndio maana yake
 
naelewa ni mtu anayechinja watanzania wanaoongea ukweli na kuzuia vyombo vya habari vinavyotoa habari za ukweli na kutaka kila mtu amtukuze yeye hata kama anakosea hiyo ndio maana yake
Huelewi hata mantiki ya hoja yangu.

Uwezo wako wa kuchanganua hoja ni mdogo sana.

Nadhani nitakuwa napoteza muda wangu na wako kama nitaendelea kujibu maandiko yako.

Samahani kama nitakukwaza kutokana na angalizo langu!
 
Amani ya Tanzania inatokana na ubwege wa Watanzania wenyewe. Yaani kiongozi ana tukana wananchi wake na wapo wanacheka nae tu heee.

Nasubiri mafuta yakipatikana Tanzania nione hio amani ya Imani za dini kama ipo kweli. Angalia Nigeria, Sudan na nchi zote zinazozalisha mafuta Afrika utajua nini naongea hapa.

Ndukiiiii
 
Hapo Ndio AKili Yako Imeishia Kushindwa Kujenga Hoja Kusikufanye Useme Mwingine Hana Uelewa Juu Ya Hoja Husika

Kumbuka Kama Mwalimu Kashindwa Kumfundisha Mwanafunzi Basi Kavamia Fani Hapo Ndio Kama Wewe

Tatizo Unasoma Kwa Kukariri Hausomi Kwa Kutaka Kuelewa Mwandishi Alikuwa na Lengo Gani

Hebu Rudi Tena Shule Ukasome Nini Maana ya Uchambuzi Ukachambue Na Hadithi Za vitabuni Kisha Urudi Mezani Kuleta Hoja Zako

Siku Nyingine Toa Hoja Yako Unavyoelewa Sio Useme Fulani Hawezi Kujenga Hoja Hiyo Ni Nidhamu Ya Uwoga Katika Midahalo Maana Yake Hautaki Kukosolewa
Bali Utukuzwe Tu Kwa Kauli ZAko Hata Kama Ni Mbovu.

Na Hiyo Maana Ya Uongozi Niiyokupa Ndio Maana Halisi Kwa Hapa Nchini Kwetu Kama Unabisha Ungeleta Maana Yako

Kasome Tema Elimu Bure Naona Hata Jina Lako Hauendani Nalo Sasa

Msema Kweli Hana Nidhamu Ya Woga Kama Yakwako Jenga Hoja Kuvunja Hoja Usilete Tantalinta Za Kusema Haujui Kujenga Hoja

MIe Ndio Kijana Huru SAwaaaaa?
 
Amani ya Tanzania inatokana na ubwege wa Watanzania wenyewe. Yaani kiongozi ana tukana wananchi wake na wapo wanacheka nae tu heee.

Nasubiri mafuta yakipatikana Tanzania nione hio amani ya Imani za dini kama ipo kweli. Angalia Nigeria, Sudan na nchi zote zinazozalisha mafuta Afrika utajua nini naongea hapa.

Ndukiiiii

Hapo Ndio Watajua Watanzania Tunamwabudu Mungu Ambaye Ni Jemedari Wa Vita Sasa
 
Unajua Tanzania Ingekuwa Nchi nyingine basi Mda huu tungekuwa Tunasikiliza milio ya mitutu kama miziki na huku tukishuhudia samu za watu kila kona kama machinga pale stand ya k/koo.
Hakuna Kiongozi Atakayejisifu Kuwa Anasimamia Amani Tanzania ama Kaiweka Amani Tanzania.
NARUDIA TENA HAKUNA KIONGOZI ANAYEPASWA KUJISIFU KUWA ANASIMAMIA AMANI TANZANIA.
Maana viongozi wao ndio wanakuwa wakwanza kuvunja amani kwa namna ya Uongozi wao
Tumshukuru Mungu Kwa kuweka Tanzania Ya Wakristo Walioshika Dini Na Waisilamu Walioshika Dini.
Tukiona Serikali Inavyotuzungusha Yaani Tukiwaza vitabu Vyetu Vitakatifu Basi Tunafumba Macho Na Kuvumilia Yote.
Kiongozi Wewe Unayesema Unasimamia Amani TANZANIA nakuambia KWeli Watanzania TUna Hofu Ya MUngu Ndio Maana Tunatulia Ila Hauna Hata Chembe Ya Kusimamia Amani.
Kuamua Kufa Kwa Ajili Ya Nchi Yetu Inawezekana Kabisa Ila Tunawaza Mungu Anatuusi Tuishi Kwa Amani.
Watanzaia Wenzangu Na Tuzidi Kushika Dini Zetu Ili Tuitunze Amani Yetu Zaidi Na Zaidi, Amani Yetu NI Sisi WEnyewe Tulio Nayo Wala Sio Kiongozi Yeyote maana Tukiasema Tutakufa Kwa Ajili Ya Nchi Yetu. Hata Kwa Mitutu Ya Bunduki Hakuna Wa Kutusimamisha.
Viongozi Wanatupoteza sisi wenyewe na hawajui damu za watu wasio na hatia zinatutia kichefu chefu NA Hawajui Zinaweza Kututapisha Na Wajifanya Wansimamia Amani.

Kwakweli Amani Tunayo Sisi Wenyewe Wananchi Kwakuwa Tunahofu Ya MUNGU Na WAla Hatuna hofu ya Kiongozi Hata Akiwa anatuchinja usiku kama kuku wake waliobandani.

Amani Yetu Tanzania Tunayo Sisi Wenyewe Wananchi Tuzidi Kumcha Mungu Kwa Dini Zetu Zote Ili TUzidi Kudumu Katika Amani Yetu.

AMANI YA TANZANIA INASIMAMIWA NA WATANZNIA WENYWE NA WALA SI KIONGOZI

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE NA UWASAMEHE VIONGOZI WANAOONA SISI WATANZANIA NI SAWA NI KUKU ZAO TENA ZILE BLOILER

Yamekuwa hayo tena nilifikri Amani yetu iko mikononi mwa fisadi Lowasa kwa maana alisema mnasubiri tamko lake mkinukishe!
 
Yamekuwa hayo tena nilifikri Amani yetu iko mikononi mwa fisadi Lowasa kwa maana alisema mnasubiri tamko lake mkinukishe!

Kuna Wakati Machafu Yanapofanyika Watanzania Huwa Yanatukera sana Inatufanya Kutokana na Hasira TUchukue Maamuzi Yasiyo Sahihi Ama TUnazungumza Jambo Lolote Ambalo Sisi TUnaona Linatufaa Lakini Tukisha Kumbuka Kuwa Tuna Hofu Ya Mungu Ndani Yetu Tunaamua Kutulia Na Kuacha Wacha Tukae Kimya Tu.

Pia Jua Hapa Sijazungumza Cha Lowasa Ama Nani Nimeongelea Sisi Watanzania Kiujumla Nadhani Ukirudia Kusoma Unaweza Pata nini Nimezungumza
 
Hivi kuna uchaguzikweli 2020 au ni kubariki tu waliopo waendelee? Ikiwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makada na wana usalama, mhh hapo kuna uchaguzi kweli? Ikiwa makasuku wa iliyokuwa tume ya katiba mpya ndo haoo hivi kuna tume huru kweli ya uchaguzi? mbona naona kama kuna shetani tayari ndani ya masanduku ya kupigia kura kabla ya 2020? Hivi wananchi wetu hawafanini na watunisia, libya, misri, yemen n.k? Kwanini Ghana waliweza? kwanini Kenya wameweza? Mbona siasa zetu zinakimbilia kunako Rwanda, Burundi na Uganda? Mbona tunasonga bila katiba tena sasa ni jeshi la mtu mmoja? mhh......yahitaji roho ngumu kurudi Tz
 
naunga mkona hoja 100%, ni uongo wa waz kiongoz yoyote akicmama akasema ye ndo anaitunza aman yetu watz. pia historical bakgraund inaonesha watz ha2kuwa na machafuko makubwa ya kikabila, kdin na kikanda kma nch nyngne. Naamin watawala ndo watakaokuja kuiharb aman yetu na sio upinzan, upinzan upo kwa ajil ya kukosoa na kushaur selkar
 
HIVI NJAA YAWEZA FANYIWA UTANI SIKU HIZI? AU NI KEJELI ZA WALIOSHIBA?
Kumekuwepo na tetesi hapo nchini kwetu za kuwepo kwa janga la njaa, jambo ambalo limekanushwa kwa kauli kali na Rais wetu katika mkutano wake pale Bariadi. Pamoja na kwamba tuko nje ya nchi yetu lakini tunaona si jambo jema kukanusha ukweli wa tukio kubwa kama hilo, hususani kama limesha anza kujitokeza au kuwepo kwa dalili za njaa. Ni wazi tunao ndugu, jamaa na marafiki pia ambao wameanza kutupigia yowe la kuomba msaada kwa hali ilivyo sasa nchini kwetu. Naomba siasa iwekwe pembeni kwanza, taarifa sahihi zikusanywe kwa haraka kupitia vyanzo vya serikali tujue ukubwa wa tatizo na huduma ya dharura ianze kutolewa kwa wahanga. Maneno hayana tija Ikulu ya Dar es salaamu inaongea mno sasa tunahitaji utekelezaji wa haraka katika hili.

Wanao mshauri Rais waache kumpotosha kwa sababu ya hofu ya kulinda vyeo na madaraka yao, itakuwa aibu kubwa kwa taifa linalojinasibu usiku na mchana kuwa uchumi wake umepanda wakti wananchi wana lala njaa na maisha ni duni. Nawasihi Mawaziri na viongozi waandamizi waache kumwogopa Rais. Rais ni raia tu tuliye mpa heshima na madaraka ya kutuongoza, ana haki zake kikatiba kwa sababu ya demokrasia hiyo, lakini Wananchi kama waajiri wake wa mwisho tuna haki ya msingi ya kumwonya na kumrekebisha na asipokuwa msikivu tuna haki ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake. Na hayo ndiyo mamlaka ya kikatiba ya wananchi yanayo tajwa na katiba yetu. Kwa hiyo suala la njaa siyo jambo la ku compromise, Rais isikemee tu na ijiridhishe kwa kufika na kuona kwa macho yake huko kunako tajwa kuwepo kwa matukio ya njaa na huo ndio utumishi tunao uona hapa ughaibuni. wenzetu hapa janga dogo tulikitokea utaona breaking news na wakuu wote wa serikali wako pale kutafuta suluhu mpaka tatizo liishe.

Mwisho ni shauri serikali yetu iwekeze kwa kiwango kikubwa sasa katika kilimo cha umwagiliaji kupitia ziwa Victoria, lukwa, tanganyika, nyasa na mito mikubwa. kuna mahitaji makubwa mno ya chakula duniani kuliko wakati wowote na ni biashara ya uhakika zaidi kuliko kukimbilia hivyo viwanda tunavyodhani. Kwa ujumla mapinduzi ya viwanda yanaanza na uwekeaji mpana katika elimu, elimu na elimu maana yake ni rasilimali watu wenye ujuzi wa kubadili rasilimali ghafi kuwa bidhaa mbali mbali. Pili mitaji, tatu miundo mbinu na mwasiliano, nne masoko, tano sera na sheria n.k.

Kama mikoa inayozunguka maziwa nilo taja ingekuwa na scheme kubwa za kilimo cha umwagiliajia na Bonde la Morogoro likafanyiwa kazi vizuri tungeaga umasikini haraka sana
Kuna upungufu wa zaidi ya asilimia 47% ya chakula duniani sasa, hata hapo jirani kenya wana hitaji chakula, sudan, ethiopia, eritrea, somalia,chad,afghanstan, iraq, lebano, syria n.k yaani kweli hatuoni soko hilo lisilo na mashariti?

Asanteni wana jamvi
UFO-Ughaibuni
 
Mleta thread anachekesha kweli eti Watanzania tu wachamungu sana ndo maana tuna Amani.

Dunia Nzima Watanzania ndio watu Wenye ujasiri wa kuchuna Ngozi ya Mtanzania Mwenzao kwa kuwa tu wanataka wawe Matajiri

Dunia Nzima ni Watanzania pekee ndio Wana ujasiri wa kumchoma Moto Bibi kizee wa Mtaani kwao kwa kuwa tu Macho yake yamekuwa mekundu kwa uzee na shurba za kupikia kuni eti ni Mchawi wa Maendeleo yao.

Hii Amani ni Matokeo ya Sera za Serikali Pamoja na Uungwaji Mkono wa Serikali toka kwa Wananchi.

Wahuni wachache toka Pemba wangelegezewa 2001 AMANI ingekuwepo?
 
Kinacho weka amani ni uoga na uzembe wa watanzania. Si juzi tu hapo vijana wadogo wanajiita panyaroad waliiba na kupora mali zenu mchana kweupe tena mjini kabisa alafu wanaume wazima na pumb.u zenu mkakimbia mbio. Pumbafu hamuwezi hata kujilinda wenyewe mtaweze kulinda maslahi ya nchi?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom