Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,315
- 6,845
Kinaniuma sana. Kinakaa kinapigwa pigwa tu na kukaa kinafokewa fokewa ovyo ovyo tu kila mara bila sababu. Kwa mtizamo wangu hicho kipo kwa ajili ya kuburudisha na au kufundisha watoto. Mtoto anahitaji kupendwa, japo haimaanishi asikanywe au kuchapawa viboko, kama amekosea. Lakini sasa hiki kidori hakijakosea wala kufanywa unastukia kinaanza kuchapwa makofi au kufokewa! Sasa masanja anawafundisha nini watoto wetu hapa kama kidori alichokileta ili kiwaburudishe anakipiga au kukifokea bila hata kuwa kimemkosea? Mimi nadhani hapa hapa haki za watoto wetu zinakiukwa. Ningeshauri wakiondoe kwenye jukwaa au aache kuki-misstreat namna hiyo. Nadhani hata watoto walio wengi watakuwa hawafurahii kabisa hali hiyo!