Fredinho
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 971
- 1,160
Yanga kwa sasa inamiliki makocha wanne bora afrika mashariki.Baaada ya uteuzi wa Lwandamila kuwa kocha mkuu wa Yanga klabu hiyo kongwe na maarufu nchini ilimteua aliekuwa kocha wake Hans Pluijm kuwa mkurugenzi mkuu wa ufundi klabuni hapo,majuzi hapa mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga Charles Boniphace Mkwasa ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo,hawa watatu pamoja kocha msaidizi Juma Mwambusi wanaifanya Yanga kuwa na makocha wanne bora kwa wakati mmoja.
Mimi naamini sababu kubwa ya Yanga kufanya hivyo ni uoga,Yanga wanahofia Lwandamila hawezi kuwafikisha wanapotaka na wakati atakapoondoka wataingia gharama nyingine kutafuta kocha mwingine,ndio maana wameamua kuwabakiza kundini Mkwasa na Pluijm ambao kwa pamoja walifanya kazi nzuri sana Yanga na wanaonekana kuelewana vilivyo kiutendaji.
Sababu ya pili inaweza kuwa kuvikomoa vilabu vingine,inafahamika wazi kuwa Pluijm na Mkwasa ni miongoni mwa makocha wazuri sana,Yanga inahofia kuwa ikiwapoteza wanaweza kuangukia mikononi mwa wapinzani wao wakubwa hususani Azam ambao kwa miaka ya karibuni wamekosa makocha makini wenye uwezo wa kuwasaidia kupiga hatua nyingine mbele kutoka hapo walipofikia.Na kwa ubora walionao Mkwasa na Pluijm kama wakitua Azam wanauwezo wa kuifanya kuwa timu tishio zaidi kwa Yanga.Hivyo njia pekee ya kuhakikisha yote hayo hayatokei ni kuendelea kuwakumbatia makocha wao wote wanne kwa wakati mmoja.