- Source #1
- View Source #1
Wakuu huyu aliepost hii video huko TikTok anasema ni tukio limetokea kwenye mkutano wa kijiji huko Sumbawanga. Je, ni kweli?
- Tunachokijua
- Ipo video iliyochapishwa katika mtandao wa TikTok ikionesha kimbunga kilichoambatana na upepo mkali unaoonekana kuleta usumbufu katika uwanja unaoonekana kuandaliwa kwaajili ya mkutano wa watu.
Katika video hiyo inasikika sauti ikisema tukio hilo kimetokea Sumbawanga katika moja mkutano wa kijiji ambao umevurugwa na kimbunga hicho huku zikihusishwa imani za kishirikina.
Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa tukio hilo halijatokea Sumbawanga kama inavyotajwa.
Kwa kutumia Google Reverse Image Search pamoja na utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) imebaini taarifa kuhusu tukio hilo ambalo inaelezwa kuwa ni kutoka nchini Nigeria.
Inaelezwa dhoruba hiyo ya upepo ilivuruga maandamano ya watu takribani 10,000 yaliyokuwa yakifanyika katika eneo la serikali za mitaa la Oju (LGA) kuonesha uungwaji mkono kwa Rais Bola Ahmed Tinubu na Gavana Hyacinth Alia.
Upepo huo mkali ulisambaratisha mahema na viti, hali iliyosababisha vurugu na taharuki katika tukio hilo. Licha ya changamoto hiyo, waandaaji walisema wataendelea kuonesha uungwaji mkono wao kwa Rais na Gavana.
Aidha Google Earth inabainisha uhalisia wa eneo hilo lililopo nchini Nigeria na si Sumbawanga nchini Tanzania kama inavyoelezwa.