Hii technique ina mapungufu gani jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii technique ina mapungufu gani jamani?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Sangarara, Jun 1, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Ili kudhibiti Madawa ya Kulevya.

  1. Jeshi la Polisi liwakamate mateja wote waliozagaa barabarani.

  2. Mateja waliokamatwa waulizwe, wamenunua wapi unga, wanataja

  3. Maretailer waliotajwa na mateja wanakamatwa pia, sababu hata makazi yao yanajurikana.

  4. Maretailer wakiisha kamatwa na wenyewe wataeleza wananunua kwa nani?

  5. Chain inaendelea mpaka kufikia mwisho.

  Njia hii inamapungufu gani?
   
 2. K

  Khokhma Senior Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Iko vizur tatzo ni kwamba wanaotakiwa kufanya hivyo wako ndani ya mzunguko huo au wanafaidishwa na walioko kwenye huo mzunguko. Mtizamo wangu
   
 3. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  kisha wakiwakamata na unga, unaifadhiwa kwaajili ya ushahidi. siku ya kesi unabadilikuwa kuwa unga wa dona.

  Wewe una njaa watoto ada shule unadaiwa pesa kibao, kodi ya nyumba hujalipa huu mwezi wapili sasa. mshahara wenyewe unaishia kwenye madeni. KISHA UNALIKAMATA ZUNGU LA UNGA na mzigo wa 100 milioni, ukapewa 10m unyamaze kwani kuna mbaya. WEWE badilisha tu kuwa unga wa sembe, kisha maisha yanaendelea.( BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA)
   
 4. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sio kiulaini namna hiyo, hii biashara ukijitia kimbelembele kukamata hao ma-retailer, ujue umepoteza maisha. Filam mbalimbali za Kimarekani ni kama mfano hai, kama ni hivyo biashara hiyo hata Marekani ingekuwa imetoweka.
   
 5. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,467
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180

  Njia ya kupunguza biashra ya madawa ya kulevya ni;-

  1. As long as kuna'demand there must be supply. Kuelimisha vijana kwa nguvu zote madhara ya matumizi ya mihadharati tangu shule za msingi, liwe kama somo linalo jitegema. China wanaua yeyote atakayekutwa na dawa hizo, still watu wanayaingiza na ukifika china, mateja kibao wakichina.

  2. Serikali inauelewa mdogo sana wa NJIA za biashara hii, hivyo mara nyingi inategemea risasi kidole ktika kukamata hizo dawa sio NJIA, MTANDAO au TecH. Ukimkamata (pusher = retailer), na akakupeleka kwa (wholeseller = mzungu) bado nivigumu kum'connect zungu na unga hadi umkute nao, na hata huyo zungu akikamatwa bado ni kijisehemu tu wa'zungu wote. Hivyo basi, serikali lazima iingize watu wake kwenye mtandao wa wauzaji, au ambao walishaifanya wakaacha, ili wape tip ya kinachoendelea, kila siku hii biashara ina update.

  3. Serikali iahidi na itoe kiukweli kiasi kikubwa cha fedha kwa atakayepelekea kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha dawa, i.e kuanzia 1kg. Nakuhakikishia kila siku wauzaji watakamatwa, lakini tu endapo informer hatakuwa exposed.

  4. Lazima serikali ijipange kuelewa tabia na muundo wa biashara hii ili ijue inazuia nini.
  Mfano;
  i. Wapo wanaoingiza biashara hii nchini Tz, ili waipeleke nchi zingine kubwa duniani. Hawa huwa ni wafanyabiashara wakubwa sana na wenye fedha nyingi, humiliki biashara zingine kama maduka au showrum fulani ili kuzugia. Wengi wao hawana asili ya kibantu. Tabia ya Wazungu hawa ya kuingiza unga ni, kuuficha katika bidhaa fulani zinazoingizwa nchini, au kutuma watu wengi mara moja kununua, halafu watu hao huingianao nchini kupitia viwanja mbalimbali nchini hasa kia, au vya nchi jirani kisha kuingia nchini kupitia boda. Hata kama wazungu wa aina hii wakiamua kuuza unga huo hapa nchi, kati yake na retailers kuna chain kubwa ya watu wa kati, ambao hununua kwake kwajumla na kuutawanya kwa jumla.

  ii. Wenye asili ya kibantu ambao ndio hasa huuficha kwenye matumbo yao kuliko race nyingine yeyote, hawa huleta kwa ajili ya kuuza tu. Leo ana hela sana kesho hana hata kumi. Leo anatembelea bonge la gari, kesho anatembea kwa miguu, leo ananyumba, kesho anatafuta mteja aiuze..., hapo alikamatwa akakung'utishwa anauza ili aanze tena. Tabia kubwa waliyonayo ni kupoteza travelling docs, na ukifungua passport yake utakuta visa za stika hasa za nchi ambazo hajaenda au haendi, zimewekwa page za kushoto i.e page 2, 4, 6...nk ktka ppt ya sasa ili kufunika mihuri ya entry au/na exit ya nchi zenye kuzalisha. Hata mihuri iliopigwa inatabia nyingi mno ili kujua huyu yupo au la....ili afuatiliwe.

  iii. Group lingine ni pushers, hao wananuna grams kadhaa kutoka kwa wholesalers na kudeal na mateja, lakini pia humweka sub-pusher kati yake na mateja. Mateja hujua wapi walipo hawa pusher, kwani eneo moja huwa wengi ambao ni rivals, since kila mmoja ana bosi wake. Bado sio rahisi kumkamata huyu pusha, kwani hakai na unga mfukoni....mara kete kadhaa zipo chini ya jiwe lile, au juu ya paa fulani...akija teja anaenda kufukua na kumhudumia, akiondoka anachimbia kwengine. Tabia yake huwa anafedha nyingi lakini hajui amount yake ukimfuma gafla na hasa coins, ambazo mateja huzivuna kutoka kwa makondakta.

  5. Kasoro kwa Mapusha, waliobaki woote hawa wanatabia inazofanana, kuna mahali lazima waende au watume watu kwa niaba yao (siwezi kupataja humu hadharani lakni simaanishi kwa wagnga). Simu zao karibu wote, zina namba ya mtu fulani na fulani na fulani au fulani, ijapo kuwa hawa wafanyabiashara wanaweza wawehawajuani.

  Kibanga Msese
   
 6. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #6

 7. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mkuu Sangarara mbona unahangaika sana kutafuta solution?

  Hivi unafikiri Serikali haiwajui Waagizaji, Wasambazaji na Wasafirishaji wakubwa wa madawa ya kulevya? - inawajua sana

  Hizo biashara za watu wakubwa & wakubwa wana interests nazo
   
 8. The last don

  The last don JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Mkuu kuna point umemiss kuhusu hii biashara,facts ni kwamba si kuwa serikali haiwajui key playerz...kila kitu kipo wazi,issue ni kwamba ni nani atakayemfunga paka kengele.
   
Loading...