Click Hapa
JF-Expert Member
- Jan 27, 2013
- 479
- 206
Heshima kwenu Wana JF.
Nimekuwa nikijiuliza hivi nini kimetokea this time kwenye Taasisi hii ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini kwa hili wimbi la kamatakamata ya watoa Rushwa kwenye mchakato Mzima wa uchaguzi unaoendelea nchini. Kinachoshtua zaidi wanaokamatwa au kuhusishwa na kutoa Rushwa ni makada nguri wa CCM, Hata Nape?
Mpaka sasa orodha imeshakuwa ndefu: Leo nimesikia Anna Kilango Malecela naye kanaswa, hivyo kaungana na wenzie kina Chambiri, Mwigulu, Nape na wengineo.
Kama zoezi hili linaloendeshwa na Takukuru ni kwa uhalisia basi tuungane kwa pamoja kuipongeza Taasisi hii iliyo chini ya ndugu Hosseah kuwa sasa imeota MENO na inapambana vilivyo na watoa Rushwa nchini bila kujali itikadi ya nyama. Big up Hosseah na Taasisi yako.
Kwa upande wa pili inatia Shaka kuwa je haya MENO ya ghafla yameotaje, isijekuwa danganya Toto.
Kamatakamata hii naelekea kuifananisha na lile wimbi la utitiri wa watia nia wa CCM kwenye nafasi ya urais. Wajuzi wa mambo wanasema eti utitiri ule ilikuwa ni malengo maalumu ili AKIKATWA basi asilalamike kwakuwa watakuwa wamekatwa wengi kwa hiyo itabidi awe mpole tu.
Mwanzoni iliniwia vigumu kuielewa Sanaa ile ila baadaye niliielewa kuwa ndo ilikuwa maana yake, na Leo nimesikia ile Audio records ya Paul MAKONDA akimponda EL akajisahau au kwa kutokujua akapita mlemle, eti anauliza "wamekatwa Waziri Mkuu Pinda, Makamu wa rais, Mark Mwandosya n.k hakuna aliye lalamika, iweje wewe ulalamike, kwani wewe nani" kwa akili hii ya MAKONDA ni dhahiri kuwa utitiri ule wa watia nia wa CCM ilikuwa ni mpango Mzima.
Sasa hili la TAKUKURU nalo linaanza kututia hofu, hivi ni MENO ya kweli au Sanaa zilezile?
Inaweza kuwa vigumu kuielewa Nina maana gani ila nahisi hizi ni Sanaa zilezile tu, yaani siku ikitokea ikitokea Watanzania tusishangae kwa kuwa TAKUKURU ya mwaka huu imeota MENO. Watakuwa wanatwambia kuwa tayari tulishawakamata kina Nape, Anna Malecela na wengineo leo itakuwa wewe!
Maana wanasema jamaa wanatumia fedha zake kuhonga watu ili wamfuate kwa wingi. Yaani wafuasi wote walonyuma yake ni kwamba anawahonga.
Nadhani kama TAKUKURU hii imekuja kwa mpango huu ili kumvizia na hatimaye kumchafua, nadhani tayari wamechelewa sana. Ingefaa sana kama wangemnasa na kumchafua akiwa bado yupo team ile ila kule alipoelekea huwa hakuna mchezo huo wa Rushwa kama ilivyo team x na ndo maana hadi Leo hii wanaonaswa ni team x tu.
Nashauri Taasisi hii isijiingize kwenye siasa hizi chafu, ifanye Kazi kwa weledi wake tu. Watanzania wa Leo wameamka kwa kiwango cha juu sana.
Chondechonde Team Y, mna maadui wengi mno kuliko inavyoweza kuelezeka. Rushwa ni adui wa haki.