Kuja tabia ambayo watu wengi wana kuwa nayo ya kujaza chakula kingi alafu anakula kidogo anaacha kiasi kwamba wengine wanakosa. Alafu sasa bora ata ale kwa usaarabu angalau lakn mmnh anavyokula kama mtoto yanii yan kama ni wali atajaza sahan nzima alafu anauchanguachangua kisha anasema kashiba kwa kweli nachukiaga sanaa hiyo tabia
Mkuu inaonekana Leo umekosa chakula kutokana na hio tabia(joke) hii tabia kwa kweli sio nzuri me ninafikiri watu wengi wenye tabia hiyo wameathiriwa na malezi mabaya kitu kinacho wafanya wasione thamani ya chakula na kujua kwamba kuna watu wanakitafuta na wamelala njaa baada ya kukikosa
Hapana mkuu hujaelewa hapa namaanisha MTU kupakua kulingana na uwezo wake wa kula sio anapakua kwa ulafi
Nmekumbuka nlivokuaga mdogo kuna birthday party moja nlialikwa,ulivofka mda wa kula yule mama alopangwa kugawa chakula,akawa ananiruka ata sijuagi nlikua na kosa gani badae nkaona ufala nkasepa,kumbe mama mwenye birthday alikua anausoma mchezo nlivotoka nje akanifata,akawa ananibembeleza dah nkajikuta adi nmeanza kulia maza nae alikuepo na yye kumbe aliona kinacho endelea,akanifata akanipakia kwenye gari bila kuongea na mtu mpka hotelin akaniagizia misosi ile ile ilokua pale kwa birthday..ilo toka sku hyo familia ya mgawa chakula na mwenye birthday hawaelewani...kissa misosi..!!ni noma sana.
Ni kweli kabisa siyo tabia nzuri, bora hata uwe umepakuliwa utasingizia cha ajabu mtu kajipakulia mwenyewe, kama huna imani na chakula bora kupakua kidogo kujiridhisha Kama ni kitamu kikiwa fresh ndipo unaweza ongeza.
Ni kweli kabisa siyo tabia nzuri, bora hata uwe umepakuliwa utasingizia cha ajabu mtu kajipakulia mwenyewe, kama huna imani na chakula bora kupakua kidogo kujiridhisha Kama ni kitamu kikiwa fresh ndipo unaweza ongeza.
Watu wengine wakiona chakula utadhani roho inataka kuwatoka. Ubavu wa kula hawana halafu anataka kuweka mlima na wakati anajipakulia si ajabu udenda ulikuwa unamchuruzika kwa uroho wake. Watu kama hawa wanakera sana. Pakua kiasi chako ukitaka kuongeza rudi mara ya pili hata ya tatu, kumwaga chakula ni dhambi.
Ni kweli kabisa,uroho ni tabia mbaya sana,mtu akitaka kukosana na mimi amwage chakula huwa simuelewi kabisa, nini maana ya self service ni kila mtu apakue kwa uwezo Wake hata kama ni mgeni huwa nampa live potelea mbali anifikirie vibaya.