Hii somba somba ya watu, itakuwaje siku ya kufunga kampeni?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia sana kampeni za uchaguzi hususan za UKAWA na nimeona hakuna mahali popote pale ambapo watu walisombwa kwa malori na mabasi kupelekwa kwenye mikutano. Hapana wasanii, wala kupewa khanga, T-shirts na pesa, na bado Rais wetu Lowassa amezoa nyomi la kufa mtu kila mahali.

Wakati huo huo nimeona ya kuwa chama cha mafuso kimeendelea bila aibu kukusanya watu kwa malori na mabasi na kuwajaza kwenye mikutano ya kampeni ili kutoa taswira ya kuwa hata ccm inao uwezo wa kupata nyomi!

Maswali yangu ni je siku ya kufunga kampeni ya ccm Jumamosi 24.10.2015, watu wataletwa na malori? Wasiporudishwa hawa watu itakuwaje? Nyomi ya siku hiyo itatengenezwa namna gani? Kama nakumbuka vizuri kampeni ya ccm itafungiwa Mwanza, wasanii ambao wamejiandikisha sehemu mbalimbali na pengine wengi wamejiandikishia Dar es Salaam watakuwepo kwenye ufungaji? Watawahi kurudi makwao na kupiga kura? Bila wasanii kutakuwa na nyomi?
 
Tulia dawa ikuingie, kala, ney, bob jr, msaga sumu, At, wolper, barafu hawa sio wasaniiiii? Tulia dawa ikuingieee CCM inogileeeee
 
Attachments

  • 1445162807799.jpg
    1445162807799.jpg
    25 KB · Views: 312
  • 1445162897259.jpg
    1445162897259.jpg
    18.8 KB · Views: 295
Wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia sana kampeni za uchaguzi hususan za UKAWA na nimeona hakuna mahali popote pale ambapo watu walisombwa kwa malori na mabasi kupelekwa kwenye mikutano. Hapana wasanii, wala kupewa khanga, T-shirts na pesa, na bado Rais wetu Lowassa amezoa nyomi la kufa mtu kila mahali.

Wakati huo huo nimeona ya kuwa chama cha mafuso kimeendelea bila aibu kukusanya watu kwa malori na mabasi na kuwajaza kwenye mikutano ya kampeni ili kutoa taswira ya kuwa hata ccm inao uwezo wa kupata nyomi!

Maswali yangu ni je siku ya kufunga kampeni ya ccm Jumamosi 24.10.2015, watu wataletwa na malori? Wasiporudishwa hawa watu itakuwaje? Nyomi ya siku hiyo itatengenezwa namna gani? Kama nakumbuka vizuri kampeni ya ccm itafungiwa Mwanza, wasanii ambao wamejiandikisha sehemu mbalimbali na pengine wengi wamejiandikishia Dar es Salaam watakuwepo kwenye ufungaji? Watawahi kurudi makwao na kupiga kura? Bila wasanii kutakuwa na nyomi?

Nahisi bwana kiwi ...wewe sio mfuatiliaji kama unavyofikiri...
naomba uanze kufuatilia....I'll ujue ukweli ....sio ushabiki
 
Mpaka Leo Ccm Wamepoteza Jimbo La Ilemela Tena,maana Wahanga Wa Kutelekezwa Jana,wengi Walikuwa Wa Igombe, Kayenze, Bugogwa, Sangabuye,etc Nandiyo Walimfanya Kitu Mbaya Diallo 2010
 
Back
Top Bottom