Uchaguzi 2020 Hivi bado tunaamini nyomi kubwa kwenye mikutano ya kampeni ndio dalili za ushindi?

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
Habarini.

Kweli kabisa yaani mgombea akijaza nyomi kwenye mkutano wake wa kampeni kwenye chama fulani cha siasa inaashiria ushindi????

Imani gani hizi. Nimekua nafuatilia sana hapa jukwaani kila mtu anaulizia nyomi vipi huko. Tumeni picha. Sijui tunataka aerial view.
Yaani mmeyasahau yale ya Lowasa kujaza na kuambulia kuanguka.

Watu wanajazana kwa mambo mengi sana
1)kwenda kumuona mgombea live bila chenga
2) Kama kuna wasanii wanatumbuiza baasi kwenda kuburudika
3)Kwenda kupunguza stress za maisha.
4) Mtu hana kazi ya kufanya anaamua akajichanganye tu. Akija ccm anaenda, chadema anaenda. Hili kundi kubwa sana. Ajira ni shida kwa sasa.
5) kazini kwake kapewa ki memo lazima aende asipoenda hatua kali za nidhamu dhidi yake zita hukuliwa.
6)Kampeni ni tukio la historia mtu anataka aende akajionee. Miaka 5 ijayo hajui atakua wapi. Labda akhera.
7)Wachache sana wanaenda kusikiliza sera za mgombea na kuamua nani wa kumpa. Hawa ndio walitakiwa wawe wengi lkn ni kinyume.
8)..........

Kwanza ieleweke wengi wanaoenda kwenye hii mikutano unakuta hata hawatapiga kura kwa kutokua na kadi ya mpiga kura ama kutofikisha umri.

Hivyo wakuu wa vyama vyote hem tuache kujifariji na haya manyomi tusije tukaja kufa kwa pressure buureee.
 
Wakiwa wachache mmechoka wakijaa nyomi haisaidi nyie vibwengu wa lumumba mna matatizo.....iten na nyie bila usanii muone kama watakuja kupoteza muda
Mkuu naomba unitake radhi kwa kuniita mimi wa lumumba.
Mi hapa nimezungumza kama neutral.
Tena yawezekana wewe wa ufipa ndio nimeku favor maana mikutano ya ccm nyomi lazima kwa sababu imagine Diamond or Alikiba or Jeshi awepo. Sema sijui hujatumua ubongo kuni critisize?
 
Waulize CCM Kwa nini huwa wamasomba watu na mafuso kuwapeleka kwenye mikutano yao.
Show off tu. By the way ccm ina jeuri hiyo maana ilirithi miradi mingi iliyokua wakati tuko chama kimoja. So pesa ipo.
 
Swali hili linaulizwa sana pale chama cha upinzani kinapopata wahudhuriaji wengi.Vipi kuhusu wasanii kibao Dodoma?
CCM imezungumza peke yake kwa miaka mitano na waona mbali tulisema siku mkiruhusu wengine wazungumze matobo yatakuwa mengi ya kuziba.
Hapo bado Pemba!
Usiwe na wasiwasi,CCM itashinda lakini itakuwa imejifunza!!
 
Wenzako wamekodi wasanii 400+ ili kuvuta nyomi unadhani wao ni wajinga? Au unafikiri ni kwanini watumishi wanalazimishwa kuwepo kwenye mikutano ya ccm.
 
Mleta mada ni CCM, roho inamuuma
Mkuu hapa JF wewe ni mmoja wa watu nasoma sana michango yako mbona unajishusha kwa hii comment. Tulia kaa chini soma between the lines nlichoandika uone kama utakuja na hii conclusion yako.
 
Atokee Mwanasiasa Wa Chama Chochote Kwenye Hii Mikutano Ya Kampeni,Asimame Jukwaani Kisha Aseme

WANANCHI WOTE MLIOKO HAPA UWANJANI, HEBU KILA MMOJA WENU ATOE SHILINGI ELFU 5 TU AIONYESHE JUU!

Kuna Uwezekano Wakawa Nayo Wachache Mno!

Hicho Ni Kipimo Tosha Cha Hali Zetu Ngumu

Anatokea mjinga mmoja anatuambia hali za maisha ya watu zimeimarika.
 
Back
Top Bottom