Hii serikali haina mawasiliano? Na kwanini wanatenga na kutengua ndani ya saa 24

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Serikali lazima ijitazame sasa,hii siyo picha nzuri kiuongozi!

1.Jeshi la polisi linakamata(wizara ya mambo ya ndani),Baraza la sanaa la taifa linafungia(wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo),waziri (waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezo)anapangua kwa kuruhusu ndani ya saa 24.

2.Mkuu wa mkoa anavamia chombo cha habari akiwa na askari,waziri anaunda kamati,ndani ya saa moja Rais anamwambia mchunguzwa achape kazi,baada ya sikumoja kamati inamkabidhi waziri ripoti,waziri anauambia umma kuwa ataipeleka ripoti kwa wakubwa wake,ndani ya saa 24 Rias anamfurusha kazini waziri huku ripoti haijatoka.

3.Mkuu wa mkoa anatangaza kuwaondoa machinga mjini.anawapa siku za kujiandaa,.anawaaondoa tu ,ndani ya saa 24,Rais anawaambia machinga warudi mjini na kuwaambia wasaidizi wake kama wamechoka waache kazi.

4.Mkuu wa mkoa anakwenda Kigamboani,anapewa Ardhi inayodaiwa kuwa na mgogoro,baada ya siku moja waziri wa ardhi anajitokeza na kusema mkuu wa mkoa kataperia,siku moja baadae mkuu wa mkoa nae ananukuriwa na vyombo vya habari akisema mradi wa viwanda kwenye eneo lenye mgogoro lipo pale pale.

5.Waziri wa sheria na katiba anatangaza kuwa ,kuanzia sasa hakuna atakayeruhusiwa kuoa bila cheti cha ndoa,ndani ya saa 24,Rais anajitokeza na kusema,hamna mambo ya vyeti vya kuzaliwa ndiyo uoe hapana!

5.Mkuu wa mkoa anawataja watuhumiwa wa dawa za kulevya hadharani,waziri anajitokeza hadharani na kusema huu si utaratibu mzuri unaharibu brand za watu,ndani ya siku chache ,Rais anajitokeza na kusema wataje tu,hakuna cha brand hapa!.

6.Naibu Spika anawaambia wabunge suala la kukamatwa kwa wabunge ndani ya viwanja vya bunge halina zuio,siku chache boss wake(spika) anjitokeza na kusema haiwezekani mbunge akakamatwa hovyo hovyo tena bila ridhaa yake tena na afisa wa chini kabisa wa serikali.

7.Mkuu wa wilaya anamuweka ndani mwandishi,mkuu wa mkoa anawaita waandishi na kuwaomba radhi,baade mkuu wa wilaya huyo huyo anajitokeza na kusema atawatia virungu waandishi wa habari.

8.Rais anazuia michanga ya madini kusafirishwa kwenda nje,wawekezaji wanaendelea na udafirishaji wakisema wapo katika mazungumzo na serikali,spika na baadhi ya wabunge wanakwenda bandarini na katibu mkuu wa wizara,baada ya ziara hiyo tu,katibu mkuu anaondoshwa kwenye nafasi yake!.

9.Tanesco wanatangaza kupandisha bei ya umeme,waziri mwenye dhamana anajitokeza na kudai hana taarifa,Rais anatengua mabadiliko ya uongozi wa Tanesco na kuuvunja uongozi wa Tanesco.

10.Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania anasema Tanesco iwakatie umeme SMZ,baada ya siku moja Rais wa Zanzibar anajitokeza na kusema ,kateni tu tutatumia hata vibatari!

Haya mambo tunaweza kuyachukulia kirahisi tu,lakini hayaleti picha nzuri kwa utendaji wa serikali,inaonesha serikali kila mtu na lwake,kana kwamba serikalini hakuna mawasiliano!

Nachojua serikalini karibu vitengo ,idara ,wizara na sekta zote zina vitengo vya mawasiliano na wameajiri maafisa habari!

Nachojua maafisa habari wana kazi nyingi,moja ya kazi zao ni kuwasiliana na umma wa ndani na wa nje(internal and extenal public);

Najiuliza serikali inazitumia vipi idara hizi za mawasiliano serikali?je hawa maafisa habari wa serikali wanatumika ipasavyo?ama viongozi wetu hawawathamini maafisa habari na idara zao?

Maafisa habari ni muhimu sana,serikali ikijitia upofu na kuwadharanu maafisa habari ,watu wenye utaalamu na masuala ya habari,wenye kujua madhara ya habari kutoka bila kushauriana kwanza itakuwa inajivua nguo kila siku,na mwisho tutaiona serikali kama haifanyi kazi vizuri!.

Serikali iwatumie wataalam wake wa masuala ya habari,wakuu wasijisemee tu kwa wananchi bila kuomba ushauri kwa maafisa habari,pale habari maelezo kuna wataalam wa masuala haya,wizarana,mikoani mpaka halmashaurini kuna wataalamu wa masuala la habari,tunajiuliza kwa nini haya yanatokea?

Serikali ibadilike,ijitazame upya jinzi inavyotoa taarifa na kujipinga yenyewe !
 
Tatizo ni kuwa Rais ana taka kila kazi afanye mwenyewe, na wakuu wa mikoa wana copy na kupaste kwake, serikali kwa pamoja haina plan isipo kuwa plan iliyoko kichwani mwa prezda, ki ujumla nchi inakuwa haileweki nan ni nan, na nani anatakiwa afanye nn
 
Sio picha nzuri hata kidogo.. Ila ingekuwa vyema kama mtukufu angewasiliana na mamlaka iliyotoa tangazo mwanzo, na kuwaambia watangaze tena kukanusha.. Kuliko kuwadhalilisha wenzie ambao anajua kabisa hawazungushi na wala hawana ujanja wala ubavu wa kuachia ngazi..
 
utawala huu ni sawa na disfunctional family ni vuta nikuvute tu,mwenye macho haambiwi tazama lakini hapa watz msitegemee kitu sana,sote tunajua katika mazingira kama haya hamna cha maana kinachopatokana na mifano yake ipo katika jamii zetu kila pahala
 
Serikali lazima ijitazame sasa,hii siyo picha nzuri kiuongozi!

1.Jeshi la polisi linakamata(wizara ya mambo ya ndani),Baraza la sanaa la taifa linafungia(wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo),waziri (waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezo)anapangua kwa kuruhusu ndani ya saa 24.

2.Mkuu wa mkoa anavamia chombo cha habari akiwa na askari,waziri anaunda kamati,ndani ya saa moja Rais anamwambia mchunguzwa achape kazi,baada ya sikumoja kamati inamkabidhi waziri ripoti,waziri anauambia umma kuwa ataipeleka ripoti kwa wakubwa wake,ndani ya saa 24 Rias anamfurusha kazini waziri huku ripoti haijatoka.

3.Mkuu wa mkoa anatangaza kuwaondoa machinga mjini.anawapa siku za kujiandaa,.anawaaondoa tu ,ndani ya saa 24,Rais anawaambia machinga warudi mjini na kuwaambia wasaidizi wake kama wamechoka waache kazi.

4.Mkuu wa mkoa anakwenda Kigamboani,anapewa Ardhi inayodaiwa kuwa na mgogoro,baada ya siku moja waziri wa ardhi anajitokeza na kusema mkuu wa mkoa kataperia,siku moja baadae mkuu wa mkoa nae ananukuriwa na vyombo vya habari akisema mradi wa viwanda kwenye eneo lenye mgogoro lipo pale pale.

5.Waziri wa sheria na katiba anatangaza kuwa ,kuanzia sasa hakuna atakayeruhusiwa kuoa bila cheti cha ndoa,ndani ya saa 24,Rais anajitokeza na kusema,hamna mambo ya vyeti vya kuzaliwa ndiyo uoe hapana!

5.Mkuu wa mkoa anawataja watuhumiwa wa dawa za kulevya hadharani,waziri anajitokeza hadharani na kusema huu si utaratibu mzuri unaharibu brand za watu,ndani ya siku chache ,Rais anajitokeza na kusema wataje tu,hakuna cha brand hapa!.

6.Naibu Spika anawaambia wabunge suala la kukamatwa kwa wabunge ndani ya viwanja vya bunge halina zuio,siku chache boss wake(spika) anjitokeza na kusema haiwezekani mbunge akakamatwa hovyo hovyo tena bila ridhaa yake tena na afisa wa chini kabisa wa serikali.

7.Mkuu wa wilaya anamuweka ndani mwandishi,mkuu wa mkoa anawaita waandishi na kuwaomba radhi,baade mkuu wa wilaya huyo huyo anajitokeza na kusema atawatia virungu waandishi wa habari.

8.Rais anazuia michanga ya madini kusafirishwa kwenda nje,wawekezaji wanaendelea na udafirishaji wakisema wapo katika mazungumzo na serikali,spika na baadhi ya wabunge wanakwenda bandarini na katibu mkuu wa wizara,baada ya ziara hiyo tu,katibu mkuu anaondoshwa kwenye nafasi yake!.

9.Tanesco wanatangaza kupandisha bei ya umeme,waziri mwenye dhamana anajitokeza na kudai hana taarifa,Rais anatengua mabadiliko ya uongozi wa Tanesco na kuuvunja uongozi wa Tanesco.

10.Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania anasema Tanesco iwakatie umeme SMZ,baada ya siku moja Rais wa Zanzibar anajitokeza na kusema ,kateni tu tutatumia hata vibatari!

Haya mambo tunaweza kuyachukulia kirahisi tu,lakini hayaleti picha nzuri kwa utendaji wa serikali,inaonesha serikali kila mtu na lwake,kana kwamba serikalini hakuna mawasiliano!

Nachojua serikalini karibu vitengo ,idara ,wizara na sekta zote zina vitengo vya mawasiliano na wameajiri maafisa habari!

Nachojua maafisa habari wana kazi nyingi,moja ya kazi zao ni kuwasiliana na umma wa ndani na wa nje(internal and extenal public);

Najiuliza serikali inazitumia vipi idara hizi za mawasiliano serikali?je hawa maafisa habari wa serikali wanatumika ipasavyo?ama viongozi wetu hawawathamini maafisa habari na idara zao?

Maafisa habari ni muhimu sana,serikali ikijitia upofu na kuwadharanu maafisa habari ,watu wenye utaalamu na masuala ya habari,wenye kujua madhara ya habari kutoka bila kushauriana kwanza itakuwa inajivua nguo kila siku,na mwisho tutaiona serikali kama haifanyi kazi vizuri!.

Serikali iwatumie wataalam wake wa masuala ya habari,wakuu wasijisemee tu kwa wananchi bila kuomba ushauri kwa maafisa habari,pale habari maelezo kuna wataalam wa masuala haya,wizarana,mikoani mpaka halmashaurini kuna wataalamu wa masuala la habari,tunajiuliza kwa nini haya yanatokea?

Serikali ibadilike,ijitazame upya jinzi inavyotoa taarifa na kujipinga yenyewe !
Maamuzi ya Serikali ni Shaghala Baghala! No Coordination! We Need a System, Not a 1-Man Show

Paskali
 
Maamuzi yote ya kuingilia utaratibu yanafanywa na mtu mmoja, bila kufuata utaratibu wowote unaoeleweka.

Unategemea nini?
 
Kweli nyumbu ni nyumbu hawajui kuwa Rais anayo mamlaka ya kutengua agizo lolote lile...wimbo ungeendelea kufungiwa wangeendelea kupiga kelele
 
Sio picha nzuri hata kidogo.. Ila ingekuwa vyema kama mtukufu angewasiliana na mamlaka iliyotoa tangazo mwanzo, na kuwaambia watangaze tena kukanusha.. Kuliko kuwadhalilisha wenzie ambao anajua kabisa hawazungushi na wala hawana ujanja wala ubavu wa kuachia ngazi..
AWAMU ILIYOPITA YA JK HAYA HAYAKUJITOKEZA SANA. TULISHAURI,KUWE NA SEMINA ELEKEZI HASA VIONGOZI WAPYA! ISSUE YA GHARAMA ZA SEMINA KWA VIONGOZI MARA KWA MARA ISIWE SABABU YA VIONGOZI KUSHINDWA KUKAA PAMOJA NA KUELEKEZANA. HUKU MAWILAYANI NDO BASI TENA,KILA MTU KIVYAKE.
 
Tabia hii ya kukanusha kauli za viongozi hadharani, itawajengea viongozi/watendaji nidhamu ya uoga, na kuwafanya wasiweze kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
 
Ona man show. Kamata achia huru, teua futa uteuzi fanya ziara ya kisanii Bandari au uwanja wa ndege.
 
Back
Top Bottom