Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,526
- 37,841
Wiki hii imeshuhidia watu wawili wanaopaswa kuheshimika kwani ni Wabunge wakitoa maoni yanayopaswa kutolewa na Mjukuu wa mhusika anayesoma chekechea.
1. Wa Kwanza kupiga Boko alikuwa Mbunge wa viti maalum CCM Ng'wasi Kamani. Bila kujali Watanzania wanapitia magumu yapi kimaisha akapendekeza Kwa Waziri Mkuu ichapishwe noti yenye picha ya aliyemuita "Mama yake" yaani Rais Samia. Hakujali gharama wala athari za kuongeza noti mpya kwenye mzunguko wa uchumi. Kwa vile lengo ni kumfurahisha mama yake akatwanga hivyo hivyo.
2. Wa pili huyu ndo kiboko. Kwanza amekuwa mwalimu Kwa Muda mrefu na kisha akabahatika kuwa mke wa Taifa mwaka 2005 kabla ya kuwa Mbunge wa viti maalum mwaka 2017 na baadaye "akapewa" Jimbo 2020. Huyu akapiga chanua Kwa kusema gauni la Mh. Samia ndo liwe vazi la Taifa. Yaani kuanzia Sasa nchi ione Kila anachovaa Samia kama cha kitaifa.
Hivi mawazo haya huko bungeni huwa wanayapata humo humo au Mbunge anatafakari nyumbani au ofisini anashirikisha wapiga Kura wake na kwenda na hoja mbovu kama hizi?
Hivi hiyo Party Cocas huwa ina kazi gani kama wanachama wao wanaongea kama Kuku wasio na kichwa bungeni?