JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
kwani na huyu katika picha nae zamani alikuwa anapewa vitafunwa na wakubwa?alianza zamani kuwa dhaifu.Kweli watu tunatoka mbali tena tukiwa dhalili wa kusaidiwa lakini Mungu akitukumbuka tunajisahau na kuwa jeuri,tuombe Mungu atusamehe hatujui tutendayo.
Hapa ofisini kwetu kuna kijana aliajiriwa alianza kama intern asubuhi alikuwa anakuja anaanza kazi mnyonge nikawa namuuliza vipi akaniambia akila chakula hapa kazini mchana ndio mpaka kesho yake mchana hapa kazini tena. Ikifika week end ndio anakuwa na mawazo mara dufu atakula wapi na kipato ni kdogo sana.
Tulikuwa tunamfanyia hisani ya pesa ya vitafunio na wakati mwingine tunamuongezea share zetu za chakula lakini baada ya kupata ajira ya kudumu imekuwa tabu tupu.Anatusumbua na kacheo alikopewa na anawasumbua sana intern wenzie wanakuja hapa, huwa namuangalia sipati jibu.