Y amegombana na X. Katika ugomvi wao Y amemtishia X kumuua, katika kuhofia usalama wake X akaamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa kuwa Y ametishia kumuua. Y akaitwa kituo cha polisi na kuhojiwa na kupewa onyo na angalizo kwamba ikitokea X akafariki katika mazingira ya kutatanisha basi Y atawajibishwa. Sasa siku moja Y akiwa barabarani anaendesha gari na X akiwa natembea kwa miguu ikatokea ajali Y akawa amemgonga na gari na X akawa amefariki dunia. Y akakamatwa na kufikishwa kwenye kituo cha polisi. Sasa tatizo langu ni kwamba Y atafunguliwa kesi gani TRAFFICK CASE au MURDER CASE?