Poleni na majukumu ndugu zangu,.naomba kuuliza jamani naombeni msaada wenu wa mawazo;
Hivi mwanaume akiwa na mpenzi wake, ambaye anampenda na wameshafika mbali kama kuchumbiana na kushirikishana kwenye mambo mbalimbali yanayowahusu,sasa kama mmesha chumbiana si inamaana mko mbali zaid yaani kuwa mume na mke soon??
je ni sawa kwa huyo mwanaume kumhudumia huyo mpenzi wake kwenye mambo kama, kulipa kodi mbalimbali kama nyumba,kusaidia ndugu za mpenzi wake huyo,kumhudumia huyo mpenzi wake kuanzia chakula mavazi n.k, na mambo menginemengine tu.? na wakati bado hawajafunga ndoa? au bado hata hawajapelekana kwa wazazi? hapa naona shida wamechumbiana vipi bila kwenda kwa wazazi ama siku hizi kidigital mnachumbiana chumbani peke yenu??
inawezekana kweli huyo mpenzi akawa kimaisha hajakaa vizuri bado labda ndo anatafuta lakini mi napenda kujua jamani ni haki ya mwanaume kumfanyia mpenzi wake hivyo? kutoa ni moyo wa mtu ila tu wewe mpokeaji ndio inakubidi uwe na akili za ziada kwamba kwann upokee zawadi tu toka kwa patna wako?? je wewe huwa unatoa nini inreturn?? ama wewe ni mkono wa birika?? so far kwenye uchumba ni mapema sana kuexpose shida za familia yako kwa spouse wako. mm huwa naamin katika jambao moja tu kwamba ukitaka heshima toka kwa mchumba wako kwa wazazi wako basi asijue udhaifu wao yaani hata kama ni maskini basi wawe jeuri manake mkiruhusu pesa yake ikaisemesha familia basi inaeza ikageuka makaa ya moto kwenu nyote.
na vice-versa jamani nisiwe biased.. ahsanten