Hii ni kawaida kwa watoto au?

Hii ni kawaida kwa watoto au?

lusban

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Posts
727
Reaction score
360
Habari zenu wakuu.

Hapa mtaani kwetu kuna mtoto wa miaka miwili, ila kwa miezi sita sasa najaribu kumfuatilia hajawahi kukosea kuvaaa viatu vya aina yoyote anavyopewa ili avivae.

Hivi hii ni kawaida au?
 
ni kawaida huyo anaelimika haelimishwi anasifa ya kujitambua ,embu niambie tabia zingine anapenda nini kingine??
 
kingine anapokuwa na watoto wenzie huwa anapenda kucheza peke yake zaidi kuliko kucheza nao.
 
habari zenu wakuu.
hapa mtaani kwetu kuna mtoto wa miaka miwili, ila kwa miezi sita sasa najaribu kumfuatilia hajawahi kukosea kuvaaa viatu vya aina yoyote anavyopewa ili avivae.
hivi hii ni kawaida au?

Mkuu mtoto wa miaka miwili ambaye hana abnormalities zozote hawezi kushindwa kuvaa viatu vyake mwenyewe.

Ni kawaida kabisa.
 
kingine anapokuwa na watoto wenzie huwa anapenda kucheza peke yake zaidi kuliko kucheza nao.

anajaribu kudadisi mazingira,kwamba kwanini kupo hivi,hiki ni nini,kwanini kinafanya hivi ,kimetoka wapi halafu haya maswali anakuwa nayo akitafuta ufumbuzi??
 
Mkuu mtoto wa miaka miwili ambaye hana abnormalities zozote hawezi kushindwa kuvaa viatu vyake mwenyewe.

Ni kawaida kabisa.

mkuu uko sawa kabisa ila huwa naona wengine hadi miaka minne bado wanachanganya cha kushoto kinavaliwa kulia na cha kulia kinavaliwa kushoto.
 
Sorry mwanajamii..its normal i was a left handed until standard two then i changed to right hand and I could still wtite with both hands..mpaka standard seven..Bi mkubwa alinipeleka hadi hospitali kwa pschoycologists even one of these brain docs at Muhimbili,kuna daktari mmoja akahisi niko na dyslexia.cause nilikuwa na handwriting mbaya..isiyo na consistency na nilikuwa poor in numbers..lakini baadaye nilipona tuu..
Mengine siwezi sema hadharani cause its kind of personal..lakini

She dedicated her time,love,affection and motherly passion to correct all those issues..but mbaya sifahamu kama wewe ni mama au baba lakini mpe muda wako and some good attention to details kama ulivoona polepole utaona mabadiliko ila kama kuna shida nyingine za ziad a kaone wataalamu watakusaidia..

Niwie radhi kwa mkorogo wangu wa kiswangilishi..
 
mkuu uko sawa kabisa ila huwa naona wengine hadi miaka minne bado wanachanganya cha kushoto kinavaliwa kulia na cha kulia kinavaliwa kushoto.

heri hiyo miaka minne..
kuna mmoja ana miaka tisa na bado hajui kiatu kipi cha kulia wala kushoto
hajui rangi ipi nyeusi, nyeupe wala blue au nyingine yoyote!
sijui ana mtindio yule!!!
 
Tena ni wa kike me mpaka nashindwa kutabili itakuaje kila mala anajichungulia kikijoleo chake
 
Nimesahau sababu ila niliwahi kuona hicho kitu kwenye somo la saikolojia kwenye stage ya ukuaji ya preoperational (miaka 2-6). Mtoto wa miaka miwili anaweza kuvaa viatu sawasawa ila mtoto huyo huyo akikua kidogo anaweza kuanza kugeuza viatu na baadae kuendelea kuvaa sawasawa. Nimesahau maelezo ya kisayansi.
 
Hata wangu ( she is 2yrs) Sijawai muona anakosea kuvaa ndala au viatu.Hii kitu nshajiuliza lakini nkahisi ni kawaida tu.
 
Back
Top Bottom