Hii ni hali ya hatari kwa uchaguzi ujao!

Hii ni hali ya hatari kwa uchaguzi ujao!

wabuyaga

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,681
Reaction score
591
Ndugu wana JF,
Inatia wasi wasi mkubwa kuwa hata kabla ya uchaguzi kutakuwa na maandamano ya hapa na pale kutokana na watu walio wengi kukosa kuandikishwa. Na hii tutaiona baada ya siku saba zilizowekwa na tume ya UCHAGUZI!
Kwa sisi ambao tupo Mikoani/Vijijini, kwa kweli hali ni ya hatari sana.
Haiwezekani watu zaidi ya asilimia 85 mpaka sasa hawajajiandikisha katika sehemu zlizotengwa halafu mseme Taifa litakuwa salama baada ya kujiandikisha!

OMBI LANGU:
Bila kuangalia ni chama gani tusipoangalia hii hali itatupeleka kule ambako hatutaki kwenda.
Haina maana yoyote wana siasa kuhamasisha kujiandikisha wakatti siku hazitoshi kabisa.

NAULIZA HIVI: Ni criteria ipi imetumika kusema kuwa siku 7 zinatosha kuwaandikisha watu katika sehemu zilizopangwa? Je wasimamizi wa kuandikisha wametoa report kuhusu hili tatizo?
Je viongozi wengine wa siasa wanachukua hatua zipi ili kuhakikisha hizi siku zinaongezewa mpaka watu wajiandikishe?

NASEME HIVI: Nenda ktk vituo vya kujiandikisha uangalie hali ilivyo mbaya sana, wakati viongozi wapo eti wanapanga nani apeperushe bendera ya kila chama.
Nani atawachagua wakati hali ni mbaya sasa hivi huko vijijini?

ANGALI sehemu ya MULEBA na BUKOBA au KARAGWE. Kama ni hivi basi uchaguzi ujao hatuutakii MEMA.

Mungu toa onyo kwa wahusika walione hili TATIZO kabla ya mwisho wakuandikisha wapiga kura.

Wenu/Wabuyaga akiwa Kyaka.
 
Hili ni janga kubwa sana, mtu mmoja anaandikishwa kwa masaa zaidi ya mawili haiwezekani wilaya nzima kuandikishwa kwa siku 7. Tuandikishe kawaida kwani BVR zinahitaji maandalizi si chini ya miaka 3 kuandikisha wapiga kura zaidi ya milioni 24 TZ. Kama hakuna hila kwa nini tusirudi analogi kwanza mpaka uchaguzi upite? Hizi BVR zina agenda ya siri.
 
Mkuu unachosema ni kweli. Ila cha ajabu viongozi wa upinzani wanachekelea et wanasubiri kuingia ikulu! Hapa labda kuna mambo wanayajua kuliko mimi na wewe.
Labda tumuulize mpenda mabadiriko Yerico Nyerere ili atupe anayoyajua kwa hili.
Kwako mkuu Yerico Nyerere
 
Tunafanya mazingaombwe kwenye mambo nyeti sana kwa taifa
 
Back
Top Bottom