Alichaguliwa kuwa mbunge na kuteuliwa kuwa waziri katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, akiwa waziri wa nishati na madini mda mfupi tu akaumilikisha mgodi wa dhahabu wa buzwagi kwa wawekezaji, mkataba huo inasemekana ulikuwa mbovu kuliko yote iliyowekwa na serikali ya awamu ya nne ya Mhe. Kikwete , mkataba huo unaruhusu wageni wavune raslimali ya dhahabu kwenda nje na kuwaacha wazawa wakiwa ni maskini wa kutupwa, pia mkataba huo ulitiliwa sahihi nje ya nchi huko katika hotel moja Uingereza inasemekena mihuri mingine ya wizara ilisafirishwa kwenda Uingereza kufanikisha mkataba huo tata na kurudi tena Tanzania katika ofisi za wizara.
Uharaka wa kupitisha mkataba huo ulizua wingu la rushwa au 10% kiasi Mbunge wa Kigoma kusini Mhe. Zitto Kabwe kupeleka mswada binafsi bungeni kuhoji uhalali wa mkataba huo, bunge lilijadili hoja hiyo ambapo mwisho wa siku ikaonekana Mhe. Zitto Kabwe amelidanganya bunge na Mhe. Mzihir Mzihir mbunge wa Mkinga CCM akapendekeza Mhe. Zitto Kabwe afukuzwe kwenye bunge asimamishwe vikao vitatu.
Wakati Mhe.Zitto kabwe akitumikia adhabu yake na kumbuka ilikuwa mwezi wa Ramadhani mwaka 2007 Mhe. Mzihir Mzihir jioni moja hapo mjini Lindi katika eneo la SIDO barabara kuu itokayo mnazi mmoja kwenda mjini Lindi alipata ajali mbaya ya gari alilokuwa anaendesha mwenyewe kiasi mkono wake wa kulia ulikatwa na aliwekewa mkono wa bandia wakati amaelazwa akiuguza majeraha yake Mhe. Zitto Kabwe alimtembela hospitalini kumjulia hali. Baadae katika uchaguzi wa 2010 hakuweza kutetea nafasi yake na alihama kabisa mkoani Lindi akahamia Kinondoni DSM na alisema hana haja ya kumfanyia mtu kampeni yeyote tu achukue jimbo.
Haikupita muda ikabainika ule mkataba alioingia nao Mhe, Nazir Karamagi ulikuwa ni mkataba fake na alivunja taratibu fulani kuufikia basi Spika wa Bunge Mhe. Samwel Sitta akaifuta adhabu aliyopewa Mhe. Zitto Kabwe kwa kuwa alichomtuhumu Waziri Karamagi kilikuwa ni cha kweli basi Spika akaamulu Zitto Kabwe aanze kuhudhuria vikao vya kamati yake ya bunge na kwamba adhabu imefutwa kwa kuwa bunge ndio lilionekana kusema uwongo.
Muda si mfupi Nazir Karamagi uwaziri wake ulitenguliwa pamoja na Mhe. Msabaha na wengine katika lile sakata kuu la richmund hii ni pamoja na Waziri mkuu alipoteza wadhifa wake. Nakumbuka Mhe. Msabaha alikuwa anajazba wakati anatangaza kujihudhuru kwake bungeni alimwambia Mhe. Spika Sitta amejua kula wali wa nazi ndio shida, na Spika alimshukuru kwa comment hiyo.
Baadae Nazir Karamagi akawa tajiri mkubwa na kumiliki hisa nyingi kwenye kampuni ya TICT inayoshughurika na kutoa makontena bandalini pia alinunua magodawn ya kutunzia korosho huko wilaya ya Newala kwa ujumla mwenzetu ndo akawa ametoka.
Kudhihirisha umaskini uliotokana na mchezo mchafu wa Wazir Karamagi nenda kata ya Njengwa au Mnima huko Mtwara kwenye jimbo la Mhe. Hawa Ghasia utakuta watu maskini kweli kweli chakula wanachokula peke yake ni kivutio cha utalii maana ni unga wa mhogo mkavu aliosagwa hadi unakuwa kama mweusi hivi na mboga chilimundu dagaa zilizokaa mda mrefu , ukipita na kuwaona wanakula utaona kama wanachukua vitu vyeusi wanaweka mdomoni ni lazima utavutiwa usogee uone wanakula nini.
Huyo ndio Nazir Karamagi ashomile toka Kagera.