Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 739
Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ni moja kati ya wilaya zinazoongoza kwa ulevi hapa Tanzania ikiwa pia ni wilaya inayoongoza kwa kuwa na aina nyingi ya pombe za kienyeji duniani kote.
Ukiachana na kinywaji chao cha mbege ambacho ndicho kinachojulikana zaidi kama pombe yao ya kienyeji, zipo pia aina nyingine nyingi za pombe kama kisesei, kimorali, kiboboso, sifa, na nyingine nyingi.
Wananchi wa wilaya hii wamejikita zaidi katika matumizi ya pombe badala ya kufanya kazi za kuwaingizia kipato na waathirika wakubwa wa pombe katika wilaya hii ni vijana ambao kutwa kucha hutumia muda wao kwenye mambo ya ulevi.
Licha ya kuchukuliwa hatua mbalimbali za kutokomeza ulevi wilaya hapa hatua hizo zimegonga mwamba na hii ni kutokana na kuwa viongozi wa wilaya hii ndio vinara wa kutengeneza pombe hizi na haohao viongozi hupewa rushwa na watu ili kuruhusu matumizi ya pombe hizi haramu ikiwemo chang'aa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana mek sadick pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo waliwahi kulikemea sana suala hili la ulevi pamoja na kuwashutumu viongozi kwa kuruhusu jambo hili kuendelea kushamiri katika wilaya hii. Na moja kati ya maeneo yanayoongoza kwa ulevi katika wilaya hii ya Rombo ni pamoja na Samanga,.
Ubetu, Kahe, Lesoroma pamoja na Msinga yakiwa ndiyo maeneo vinara ya ulevi katika wilaya hii. Hivyo basi kama serikali ina nia thabiti ya kupunguza na kutokomeza ulevi katika wilaya hii haina budi kuanza na viongozi wa wilaya hii kwani wao ndo vinara wakuu kuanzia balozi wa nyumba kumi, wenyekiti wa mitaa pamoja na wasimamizi wa halmashauri.
Tuungane kutokomeza ulevi Rombo pamoja na wilaya nyingine ambazo zimeshamiri kwa ulevi kwani ulevi unaathari kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla kutokana na kuathiri shughuli za kijamii pamoja na vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa letu. TOGETHER WE CAN