42774277
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 6,833
- 8,811
Africa ndio sehemu ambayo kuna kundi la watu wengi ambao wanaumwa magonjwa yasiyoambukizwa.
Kwa taarifa za mwaka jana mwishoni 60% ya vifo vyo vinavyotokea Africa husababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa, Yaani kwa lugha rahisi ya hesabu ni kwaka katika kila vifo 100 barani Africa, basi vifo 60 husababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa.
Asilimia 60 ya vifo Afrika vinatokana na magonjwa
Kiuhalisia hizi figure zinatisha mno. Na ukija kuangalia utakuja kugundua katika hivyo vifo 60 asilimia kubwa ya hivyo vifo vinasababishwa na magonjwa ya moyo.
Magonjwa ya moyo huku Barani Africa yanasababishwa na sababu mbili kubwa.
1. Utaratibu mbovu wa ulaji wa chakula.
Africa huenda ndiyo sehemu ambayo ni ufahari mtu kuwa na kitambi au kuwa na mwili mkubwa. Hii husababishwa na watu kula ovyo.
Ulaji wa watu wengi wa Africa naweza kuufananisha na ulaji wa Nguruwe (Mliofuga nguruwe mnajua nguruwe wanakulaje). Ulaji mbovu wa chakula hupelekea mtu kuwa na uzito uliopitiliza (Obesity) na hivyo kupelekea mtu kupata magonjwa ya moyo.
2. Watoto wengi Africa huzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo.
Inasemekana barani Africa kila mwaka watoto 10,000 huzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo.
Hapo bado sijagusa watu ambao wana magonjwa mengine sugu ambayo yanawasumbua.
Kuna utafiti ulifanuika mwaka 2012 na Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, waligundua kwamba robo 3 ya watanzania wanaugua magonjwa ya moyo. Je leo hii hali ikoje?
Kwa kifupi Africa kuna kundi kubwa tu la watu ambao wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali sugu. Hawa wote wapo kwenye risk kubwa sana ya kufa endapo wataambukizwa Corona.
Na huenda ndio maana mapema wiki hii UN walisema kwamba ndani ya wiki 3 zijazo Africa itegemee kichapo kikubwa sana kutokana na virusi hivi vya corona.
Hali inaweza kuwa mbaya kuliko ambavyo watu wengi wanafikiria.