POTOSHI Hii ndiyo Kamera ya kwanza duniani?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii picha imekuwa na ukakasi kidgo
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na picha inayosambaa mtandaoni kwa vipindi tofauti ikiwa inaonesha kamera kubwa ikiwa imezungukwa na wtau kadhaa na kudaiwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa kamera ya kwanza duniani.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa picha hiyo ilikuwa ni ya Kamera kubwa ya kwanza kuundwa ulimwenguni.

Kamera hiyo iliundwa na mpiga picha maarufu wakati huyo George Lawrence aliyezaliwa 1868 na kufariki 1938. George aliunda kamera hiyo baada ya kupat dili la kupiga picha treni mpya kisasa iliyuoundwa wakati huo huku wamiliki wakitaka mabehewa yote yaonekane kwa mara moja kwenye picha hiyo.

Mwaka 1899, kampuni ya reli ya Chicago & Alton ilianzisha huduma mpya ya usafiri wa treni kati ya Chicago na St. Louis, nchini Marekani. Treni hiyo, iliyoitwa Alton Limited, ilisukumwa na treni ya mvuke yenye mpangilio wa magurudumu wa 4-6-2 na ilikuwa na mabehewa sita yaliyopangwa kwa ulinganifu kamili, yakiwemo mabehewa mawili ya kifahari ya Pullman kwa ajili ya abiria.

Treni hiyo ilivutia kwa mapambo yake ya kuvutia ndani na nje. Kutokana na muonekano wake wa kipekee, ilitangazwa kwa jina la “Treni Maridadi Zaidi Duniani” (The Handsomest Train in the World).


Ndipo George alipounda Kamera iliyokuwa na uzito wa Kilogramu 635, ikiwa na lenzi kubwa zaidi kuwahi kuundwa ulimwenguni. Kamera hiyo pia ilihitaji takribani watu 15 kuiongoza.
There is photo as a witness that Armstrong was the first person to set foot on the moon, just curious to know where was the photographer who took pic?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…