Kama kuna makosa mtarekebisha!! Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2000, Ibara ya 67; Inasema hivi kuhusu kuchaguliwa kuwa mbunge;
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na
kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote
ya Serikali.