Kuwa Mwanachama,ni juu ya mambo mawili makubwa ni juu ya kukubaliana na Itikadi na juu ya Kutimiza wajibu wako wa uanachama. Unaweza kukubaliana na baadhi ya viongozi wako jinsi wanavyoitafasiri itikadi ya chama chako na kuisimamia na unaweza kuwachukia baadhi ya viongozi wako wanavyoivuruga itikadi.
Katika Uanachama,unaweza ukachangia fedha na ukawa mdhamini na unaweza kuchangia mawazo yanayowafurahisha wanachama na viongozi na yanayowakasirisha na kuwaudhi.
Kwa kutoa mawazo yanayo kosoa sera zinazopotosha Itikadi haimanishi kwamba wewe siyo mwanachama mwaminifu.
CHADEMA inataka wanachama wanao jua kusifu uongozi wa juu,hawataki wanaokosoa uongozi.
Hebu tujadiliane juu ya maana ya nidhamu kwa tafsiri ya Kamati kuu na mwanasheria Mkuu wa Chadema.
-Shibuda aliunga mkono Posho bungeni tofauti na Msimamo wa Chama chake CHADEMA,aliundiwa kamati maalumu ndani ya Kamati kuu na Kuonywa. Selasini aliunga Mkono Posho bungeni kwa kusema ni ndogo lakini kwasababu nisizo zijua hakujadiliwa na hakua mtovu wa nidhamu ya kuto tii msimamo wa chama.
-Lema aliandaa waraka wa kumtukana Zitto kupitia JF Kumwita mnafiki kwa kutokupokea posho,alimtukana wakati Zitto bado ni naibu katibu mkuu,hapa Tundulisu na Kamati kuu hawakuona kama ilikuwa ni kuudharirisha unaibu katibu mkuu wa Zitto kama Kiongozi wa Kitaifa, lakini Waraka wa Dr Kitila na Mwigamba wenye kuelezea umuhimu wa mabadiriko ndani ya chama, eti uliwadharirisha viongozi wakuu mkt na katibu mkuu.
-Kileo (Katibu Kanda Maalumu ya Dsm) aliweza kusambaza waraka unaomchafua naibu katibu wake Zitto, kwa kuuweka kwenye blog yake. Huku akitumia kivuli cha chama kwamba umeandaliwa na chama,japo chama kiliukataa baada ya Zitto kuukataa, iko wapi ni dhamu ya Kileo kumtukana naibu katibu mkuu kwa kumchafua?
-Katibu Mkuu Slaa,akiwa mgombea urais,hakumnadi mgombea ubunge wa kyela ndugu Eddo Makata ambaye alikuwa amepitishwa na chama,zaidi alimnadi Mwakyembe aliyekuwa mgombea ubunge tiketi ya CCM. Ushahidi ni taarifa kupitia vyombo vya habari na wananchi wa Kyela 2010.,Katiba ya chama na maadili yako wapi kwa katibu mkuu kumnadi mbunge wa CCM?
- John Mrema Kwa muda mrefu ukifuatilia michango yake Jf, amekuwa akimtukana Zitto wakati Zitto ni kiongozi wake kipindi hicho chote, Kumbuka John Mrema ni Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri chadema Makao Makuu, iwapi nidhamu yake.
-Nassari(Mbunge), huyu alitangaza hadharani kwamba CHADEMA ikichukua madaraka basi Kaskazini itatangazwa kuwa Jamhuri. Japo Mwenyekiti alikanusha kwa kujua kuwa ni uhaini kikatiba ya nchi na ya chama chetu, lakini hakuonywa wala kujadiliwa na chama kwa kupotosha umma.
-Mbowe(Mkt Taifa) Amemtangaza Dr Slaa kuwa mgombea urais 2010 kabala kamati kuu haijakaa, kinyume na katiba ya chadema 2006.
-Waraka wa Dr Kitila eti umekuwa ni uhaini, mikoani na wilayani wanachama wanaungana kushindania nafasi za uongozi ndani ya chama, lakini Taifa hamtakiwi kuungana kushindania uongozi wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa.
Kwa Kusema Machache, ukianzisha ugomvi na kiongozi ambaye Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chama hawamkubali, basi utashughulikiwa mpaka uishe, Katiba, maadili ya chama hayataangaliwa.
Ukihoji, ukakosoa kiongozi ambaye anapendwa na kuaminiwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa,basi utapandishwa hadi cheo na kuitwa Kamanda.
CHADEMA isijivunie mafanikio machache yaliyopo na kuendeleza ubaguzi, chuki na fitina, historia ina mambo makubwa mawili nayo ni ukomo na mwendelezo.