Void ab initio
JF-Expert Member
- Mar 1, 2015
- 5,723
- 5,662
Katika kashfa zote zifuatazo, hakuna hata moja ambayo iliwahi kuibuliwa na kuchanganuliwa na CCM.... Zote zimeibuliwa na vyama vya upinzani na kambi rasmi ya upinzani bungeni... Tuzitazame kidogo, jiulize... Ipi ambayo haujawahi kuisikia, tutakufafanulia kwa uzuri..
(.., kabla sijataja kashfa hizo, ningependa kufahamu, ni kashfa ipi yenye sura ya ubadhirifu na ufisadi ambayo iliwahi kuibuliwa na CCM!!?)
DOWANS.. LUGUMI .. RICHMOND.. ESCROW... RADAR TANGOLD.., TOKOMEZA.. MFUKO WA COMMODITY IMPORT SUPPORT.. KIWIRA.. KAGODA... UJANGILI.. EPA.. UDA... DEEP GREEN.. BUZWAGI.. UUZWAJI WA FUKWE.. UKWEPAJI KODI.. MISAMAHA YA KODI.. MABEHEWA MABOVU.. MABILIONI YA KIKWETE.. UNUNUZI WA NYUMBA YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALY.... UNUNUZI WA MAJENGO PACHA YA B.O.T.. LOLIONDO GATE... CHAVDA NA MASHAMBA YA MKONGE.. PEMBE ZA NDOVU KWENYE NDEGE YA RAIS WA CHINA.. HATI FUNGANI.., UUZWAJI NYUMBA ZA SERIKALI.. MIKATABA MIBOVU..
uchafu wote tumeufahamu kupitia uwepo wa vyama vya kisiasa vya upinzani....., bila uwepo wao, kamwe usingesikia hata neno IPTL na kufahamu nini maana ya DOWANS...
..., Unasema kazi ya upinzani nchi hii haujawahi kuiona.. Labda umeamua kujificha kwenye kivuli chako mwenyewe, hivyo umeamua kujidanganya na kufurahia uongo wako mwenyewe..
kazi ya upinzani kwa jibu rahisi ni kukosoa, kushauri, kuelekeza na kutoa njia mbadala za namna ya kufikia kilele cha maendeleo katika nchi au taasisi husika...
Kushika DOLA ni lengo maalum la chama chochote cha siasa...
(tusichanganye mambo mawili haya.., kushika dola na kazi ya chama cha upinzani)....
Anaesema kwamba huu ni mwisho wa upinzani nchini...anajidanganya mwenyewe.., ni sawa na mtu anaepiga ngoma mwenyewe na kuamua kucheza ala za muziki anazozipiga mwenyewe....
Hakuna mwisho wa upinzani kwenye nchi ya kidemokrasia yenye vyama vingi ndani yake...
Kama unafikiri kazi ya upinzani ni kupongeza chama tawala.., unajidanganya hadharani....
Mpinzani kazi yake kubwa ni kukosoa serikali na kutoa 'Alternative way' katika ushauri stahiki...
Ukiona chama cha siasa cha upinzani kinapiga makofi kwenye kila ambalo linafanywa na serikali.., hiko chama.., kinastahili kufunga ofisi zao na kufutwa katika dawati la usajili...
.., Katika mfumo wa vyama vingi kuna udhibiti wa uendeshaji wa serikali, watu hupanga namna gani sahihi ya kuendesha nchi yao.... Katika mfumo wa chama kimoja, watu wa chama hicho huamua namna ya kuendesha nchi kwa matakwa yao binafsi..,
..., Watu wanatoa maoni na wanapaswa wasikilizwe na pia mchango kutoka vyama vya upinzani unatakiwa uchukuliwe katika kufanya uamuzi kuhusu uendeshaji wa nchi na kuwaletea wananchi maendeleo.
Mfano huu unaweza kuonyesha vizuri tofauti kati ya mfumo wa chama kimoja na vyama vingi.... (nchi ya China ni nchi ya kijamaa ambayo ina chama kimoja, chama cha kikomunisti, ni tofauti na Tanzania, hapa kuna vyama vingi vya kisiasa, mfumo rasmi wa kidemokrasia wenye vyama vingi vya kisiasa)...
Tunahitaji siasa ngumu za harakati zilizojaa mikakati kwenye tawala nyingi ambazo kimsingi hazihitaji kukosolewa.. Ambazo zinajificha nyuma ya nguvu ya dola... Nashukuru kwa upinzani kuendelea kuimarika kila uchwao.. SERIKALI IMARA INATOKANA NA UPINZANI IMARA ULIOSTAWI...
Nitakuja kuendelea baadae na kipande cha mwisho kwenye maandishi yangu haya....
Martin Maranja Masese
Mwananchi wa kawaida