Hii ndio CCM inayo wanyonga watanzania wanyonge, tumeipenda wenyewe na tunasoma namba wote

Afixa0

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
464
485
Kwenye kampeni walituambia kwamba watawatetea wananchi wanyonge, Watatengeneza viwanda, Elimu bure, uongozi bora, usalama utaimarishwa, ajira kwa watanzania nk.

BAADA YA UCHAGUZI KUISHA IKAWA HIVI
1.Mizuka ya ziara ya kushutukiza ikaanza: Ikafikia hatua viongozi wa serikali hawalali, wanawaza tu kesho wataenda kushtukiza maeneo gani--- Hiyo ikapita kama maisha bora yalivyopita.

2. Sherehe mbali mbali zikafutwa isipokuwa za MWENGE ambayo pia ukifatilia kwa ndani huwa ina ambatana na mambo ya kichama---Ikapita kama BRN na ikaisha.

3.Suala la usafi ikatiwa mkazo ndani ya siku kadhaa ikaonekana ni kero kwasababu vifaa vya usafi serikali ilishindwa kutoa kama walivyo ahidi---Hii imebaki wimbo wa mwisho wa mwezi kama mshahara mdogo wa Waalimu.

4.Ishu ya zanzibar ikaratibiwa vizuri na kuendeshwa kwa uweledi wa hali ya juu nayo ikapita kimya kimya japo mshindo wake bado unaendelea taratibu kama suala la Burundi .

3. Bomoa bomoa ikachukua mkondo mkubwa, watu wakabomolewa nyumba na kutishiwa kila kona ya nchi kama vile ni wakimbizi---Ikasitishwa kimya kimya baada ya maumivu makali kwa wananchi kama Katiba mpya ilivyositishwa bila majibu hadi kesho

4.Ikafatia TUMBUA MAJIPU: Ikafanywa kwa mbwembwe hadi madaktari na waalimu wakapigwa na wananchi wenye mihemko kutokana na kauli za viongozi. Walitumbuliwa hadi wasio na makosa mfano wafanyakazi wa NIDA.Hii nayo inaendelea kwa figisu figisu kama TFF.

5. Bunge kutokurushwa live ikafata kwa kasi kubwa, ikiambatana na kuminywa kwa haki ya kupata habari hadi gazeti la MAWIO ikafungiwa,, Licha ya gazeti la UHURU kuongoza kwa kuandika habari za ajabu kipindi cha uchaguzi 2015 hadi leo lakini bado inapeta----Hapa sheria zikapindishwa zaidi ya mikataba mibovu wanayo saini kwa kadri iwezekanavyo ili mambo yaende sawa

6.Lugumi ikawa ni skendo ya rushwa kila kona ya nchi---Ikazimwa na chura wa msanii flani hadi leo hatujui imefikia wapi kama ambavyo hatukujua hatma ya Richmond,escrow nk

7. Madawa ya MSD ukawa wimbo mpya huko mikoani---Cha ajabu, maduka ya msd yanauza dawa kwa bei ile ile sawa na maduka ya mtaani na kitu kingine cha kusikitisha madawa yanakwepo siku ya uzinduzi au ziara tu ili tuone kwamba yapo---Hii nayo ikapita na hatuoni dawa.

8. Suala la Wanafunzi wa UDOM likafata--- Ikazimwa kwa neno ******

9.Upungufu wa sukari ukafatia kwa kasi ya juu zaidi. Vitisho vya kila aina ya rangi vikatolewa kila kona ya nchi, bei elekezi ikatolewa, sukari ikawa ni dhambi kubwa Tz ukikutwa nayo----YAKAISHA kimya kimya bila suluhisho na bei elekezi ikafeli kma KILIMO KWANZA hadi kesho

10.Ishu ya Wafanya kazi hewa ikafatia na vyeti bandia----Nayo inaendelea lakini swali ni hivi, Je kipindi wafanya kazi hewa wanakwepo TZ chama gani kilikuwa madarakani na leo kuna chama gani? maana tuna ambiwa nchi imechezewa kwa muda mrefu sana, sijui imechezewa na nani kama sio wao.

11.Elimu bure ikawa ni lugha inayotumiwa na kila kiongozi wa CCM na viongozi wa serikali ili wananchi waikubali serikali kwamba inachapa kazi. Suala la madawati likawa ni ishu ya kila siku kwenye Tv na radio hadi kwenye magazeti---Badala ya elimu bure kutekelezwa na serikali kama walivyoahidi, ikawa ni kuchangia madawati kwa hiyari, maeneo mengine kama Rorya-Kata ya Rabuor ikawa ni lazima kutoa pesa ya madawati---Elimu bila malipo nayo inaelekea kupita bila kuwapa wananchi furaha kama tulivyodhani.

12.Ikafatia ujenzi wa VIWANDA vya maneno. Hapa kila kiongozi wa ccm, wanachama na viongozi waandamizi hadi leo wanaimba SERIKALI YA VIWANDA japo hatujaona hata wembe inayotengezwa Tz kwenye hivyo viwanda. Sina imani khs Viwanda kama TUME YA UCHAGUZI.

13. Suala la kuombewa viongozi wa serikali misikitini na makanisana ikafata. Tukaona uungwaji mkono wa Viongozi wa dini kila kukicha ukizidi na wakizidi kuhuburi sera za CCM kwenye madhabahu zaidi ya neno la MUNGU----Mniombee, Tumwombee ikawa wimbo mitandaoni, magazetini nk..Hili bado lipo hadi sasa. Nchi inaongozwa kwa Katiba na Sheria sio maombi, maana siwezi kumwombea aliyeshiba wakati nina njaa.

14.Ikatokea ukosefu wa mafuta taa na pika----Ikazuiliwa juu kwa juu kimya kimya ili isiwe skendo. Haikutangazwa sana ila huku mtaani hadi leo bado ni Tatizo kubwa kama mikataba ya TANESCO.

15.Bunge kuendeshwa kibabe ikawa ni ishu pia iliyochukua nafasi kipindi mambo mengine yalipokuwa yakiendelea----Viongozi wengi wa ccm wakaongea kadri walivyoweza na kuzidisha ubabe bila kutaka suluhisho...Hii inaendelea na sijui mwisho wake lini maana tushaambiwa hakuna wa kumwondoa mweshimiwa kwenye unaibu spika.

16.Ikafata ishu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa---- Hapa maaskari wakajitahidi kweli kweli kujionesha kuwa wao nao ni makada wa CCM live live..Tena hapa ikaja kauli isiyo sahihi kwamba baada ya uchaguzi ni kazi hakuna siasa. Kwa maoni yangu hata siasa ni kazi na bila siasa hautuwezi kuendelea kuwa na viongozi wa kisiasa au vyama. Na kama siasa haitakiwi baada ya uchaguzi, basi uchaguzi unapoisha vyama vifutwe ili hata CCM isiwepo Tz tena.

13. Simu zikazimwa---Hapa napo tukasubilia kwa hamu, mwishowe ni mbwembwe tu kama ujenzi wa VIWANDA- Ikapita

17. Bajeti inayo mbana mbavu mtanzania mnyonge ikapitishwa na wale wale watetezi wa wanyonge tena kwa asilimia 100 , ikiwemo ongezeko la VAT. Hili bado inatuumiza hadi muda huu.----TRA nao wakaja na suala la kutoa takwimu ya mapato waliyokusanya mwisho wa mwezi, tukaambiwa kodi imeongezeka, Cha ajabu hao hao ndio wanaosema tena kwamba serikali haina pesa sasa sijui wanakusanya nini? Na sijui trioni 29 zile za bajeti tulizoambiwa kama ni kweli au maandishi tu kwenye makaratasi.

18.Usitishwaji wa ajira ukafata kwa kigezo cha wafanya kazi hewa....Hadi leo vijana wasio na makosa ambao hawajui sakata la wafanyakazi hewa ilifanywa na nani wako mtaani hawajui hatima yao.

19.Kutetea wanyonge ikapita sasa ikabaki nitawatetea Marais wastaafu na wafanyakazi wastaafu waliotumikia taifa kwahiyo waishi kwa amani----Hii inaendelea

20. Licha ya maaskari kuwa na taarifa za kiintelijensia kwenye mikutano ya vyama vya upinzani, polisi hao hao walishindwa kuwa na taarifa za intelijensia kuhusu mauaji ya wananchi wanyonge yaliyoendelea Tz. Wakashindwa kuwa na taarifa za Gwajima hadi pale aliporudi nchini mwenyewe.....hahahahaha nayo ikapita

22. Uteuzi ulionung'unikiwa na kukosolewa kila kona kama UCHAGUZI MKUU ukafatia------Nayo imepita.

23.Sasa hivi ipo ishu ya mkutano wa CCM Dodoma----hapa hakuna taarifa za kiintelijensia na polisi wametumia kila aina ya maneno yenye rangi ya kijani na njano na vitisho kulinda mkutano wa ccm, ikifatiwa na maneno makali wa viongozi wa ccm kote Tz.

24. Tafadhali ewe mtanzania mnyonge endelea kutaja matukio mengine unayohisi yametokea, yanatokea au yatakayozidi kutokea hapa Tz yanaonesha kwamba CCM inawanyonga wanyonge

NB: Hii ni serikali ya Wanyonge...Sasa hivi neno hapa kazi tu imeisha, haitumiki, haitamkwi na haina thamani kama hapo mwanzoni. Imebaki kutumiwa na wale Mahafidhina wachache tu, maarufu kwa jina la wafia chama au wasaka tonge. Hapa kazi imekuwa kejeli mtaani kwa wenye shida na mahangaiko yaani Wanyonge.

SWALI: Hivi Tunapoambiwa nchi ilikuwa imeoza inanuka,nchi inarekebishwa, Je ni nani aliyesababisha hayo kama sio wao?

# HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA SISI WANYONGE NDIO TUNAOZIDI KUUMIA

#CCM INATUNYONGA WANYONGE.
 
Back
Top Bottom