wamkodowenye
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 261
- 290
hivi wanawake wakibeba mimba wanatufanyia makusudi au nini? Yaani hii mimba imekua kero maana kila siku inakuja na mpya mara anataka chipsy mayai, mara malta, mara sentiana, mara piza, nashangaa kwa nini asichague ugali dagaa? Kiukweli nimemchoka huyu mwanamke maana nateseka nikienda kazini unashangaa kaja juzi kanishangaza baada ya kusema mimba inatamani tuu arufu ya soksi zangu anuse najiuliza hivi wanawake mnafanya makusudi au mbona wafanyakazi wa ndani wakibeba mimba hawachagui vyakula au kudeka? Au mimba zinatofautiana? Ebu nipeni na nyie vituko vya mimba mlivyowahi kutana navyo......