Hii mikasa ya Moto kipi kimejificha

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
HII MIKASA YA MOTO KIPI KIMEJIFICHA?

Ajali haina Kinga na ajali Ni suala la kawaida Wala haishangazi sana Bali kujirudiarudia kwa majanga ya kufanana kila mwenye akili timamu huzama katika fikra.

Katika hali isiyo ya kawaida, majanga ya moto yakigusa maeneo maalumu yametamalaki kwa kipindi cha miezi hii miwili huku mamlaka zikiwa hazitaji vyanzo halisi vya majanga hayo.

Kati ya mwezi Juni na Julai, Shule mbili mkoani Morogoro zimeungua Moto na kusababisha hasara na usumbufu mkubwa kwa wanafunzi na wadau wa shule hizo

Janga Baya Zaidi Ni lile la ndani ya Tarehe za mwanzo za Julai ambapo Soko kubwa Zaidi nchini la Kariakoo liliteketea kwa Moto huku mamlaka zikishindwa kukabili Moto huo kwa madai kuwa hakukuwa na eneo la karibu la kufuata maji hayo.

Kama hiyo haitoshi, Usiku wa kuamkia leo, taarifa zimesema shule ya Sekondari Geita imeungua Moto Jambo ambalo linafanya shule hiyo kuandika historia ya kuungua Moto Mara tatu ndani ya kipindi cha siku 30.

Kinachoumiza Zaidi, badala ya mamlaka kuajibishwa, Watawala wa Geita wameonekana katika vyombo Vya Habari wakitangaza adhabu kwa wahanga (wanafunzi) waliounguliwa Mali zao za thamani sana kwani Wanafunzi wengi wanakuwa na vyeti vyao vya ngazi za chini wawapo katika maeneo ya shule za juu hivyo wapo ambao wanateketeza vyeti vyao muhimu kutokana na majanga haya

Taarifa zimeonesha mamlaka Geita mjini ikitangaza wanafunzi 11 wa shule hiyo huenda wakapoteza haki yao ya kupata elimu huku vyanzo halisi vya Moto na uzembe wa mamlaka husika kuchukua tahadhari na kudhibiti majanga haya yanayokithiri hauzungumziwi popote iwe kwa Wabunge, mamlaka zao za juu nk.

Katika hatua ya ajabu Zaidi, Leo hii inaripotiwa kuwa shule ya msingi Amani ya Handeni mkoani Tanga imeungua Moto ambao unadaiwa kuteketeza sehemu ya jengo la Darasa na ofisi ya walimu.

Naomba mamlaka husika zijipange kujiridhisha juu ya vyanzo vya majanga haya na ikabiliane nayo kikamilifu yanapotokea ili kuondoa dhana potofu inayoweza kujengeka miongoni mwa jamii dhidi ya mamlaka za udhibiti na uokoaji majanga ya moto.

Ajali Ni kawaida na haina Kinga, kijachokuna ubongo wa wenye akili kwanini ajali za aina moja tu? Kwanini Ni sasahivi? Kwanini Ni kujirudiarudia baadhi ya maeneo? Je mamlaka husika sinakabilianaje na majanga haya wakati yanapotokea?.
Tafakuri jenzi.
 
Back
Top Bottom