Hii kweli ni haki...?!!!

Hii kweli ni haki...?!!!

Noel france

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
1,159
Reaction score
1,054
Nauliza hivi; hii kweli nihaki..?!!
Kuwatoa nje wabunge tuliowachagu ili waweze kutuwakilisha kule bunge. Alafu leo wanatolewa nje kwa misingi ya mtu binafsi na taasisi yake hii kweli nihaki? Je awajui ya kwamba pindi unapomtowa mbunge flani nje,unawakosea haki wananchi wake kule jimboni kwake haki ya kuwakilishwa? Kwanini isitafutwe njia ama utaratibu mwinge mbadala tofauti na kuwatoa nje wabunge? Au wanataka wananchi wenyewe waende hukohuko kuwasilisha hoja zao bungeni? Kwa staili hii bunge lina hadhi na ulazima hupi wa kuendelea kuwepo!
Naombeni ushauri ambao mimi kama raia wa kawaida ambaye nimesababisha bunge liwepo kwa kumchagua mbunge aniwakilishe pale bungeni,je, ni atua zipi nizifuate ili kuweza kulivunja bunge?Kwani uwenda rais wangu anaweza asifanye ivyo kwa maslai ya chama chake kwa kukiepusha kutoingia kwenye uchaguzi.
Mambo yanayo nifanya kuomba ushauri kwenu wadau,ni kutokana na mambo yafuatayo:
A}ndani ya bunge hakuna haki wala sheria zinazofuatwa.
B}ndani ya bunge matusi na majigambo yasiyo na tija kwangu kama mwananchi ndio vinaongoza.
C}ndani ya bunge spika na naibu wake wanaongoza ushabiki pasipokutumia weredi wao.
D}ndani ya bunge wabunge wamekosa kuheshmiana.
E}ndani ya bunge kunabaadhi ya wabunge na mawaziri v.i.h.i.y.o wa sheria na lugha.
F}nje ya bunge chombo cha kurusha matangazo kama vile TBC kinaninyima haki na fursa ya kufuatilia matangazo kwa uhuru na mapana pasipo kukatiwakatiwa.
Namaliza kwa kusema;ivi kweli ni haki? Je nisheria zipi nizifuate ili niweze kulivunja bunge mimi kama raia wa kawaida niliye mchagua mbunge ili aniwakilishe?
 
Watanzania naombeni tuungane ili tutimize nia.
 
Njia pekee ninayo ifahamu mimi ni maandamano,ambayo nguvu ya uma ndio itakayo weza fanya siku kuwa mchana.
 
Njia pekee ninayo ifahamu mimi ni maandamano,ambayo nguvu ya uma ndio itakayo weza kufanya usiku kuwa mchana.
 
Back
Top Bottom