Hii kwa MAPOLISI TU.

BABA JUICE

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2010
Posts
426
Reaction score
54
Kuna ndugu yangu kaibiwa kaenda polisi(osterbay) kufungua file wamemtoza shillingi elfu 30 ya kufungulia file police watatu kumkamata mualifu akatoa elfu 60, na akalipia na tax shilingi elfu 25 na eti pingu hazikai kituoni hadi kwenye kotazi zao, garama yote ni shilingi 115,000/= nikajiuliza hawa polisi hawana mishaara au mishahara yao ni midogo sana....na bado wamemfanya ndugu yangu huyu mradi wanampigia simu wanaomba pesa za kumfuatilia huyo mwizi kwani hadi muda huu naandika habari hii mwizi mwenyewe hajakamatwa.....kwakweli sielewi kazi za polisi na garama zao kwani mi najua polisi ni huduma.....hata file la kesi mahakamani hufungui kwa elfu 30. Nielimisheni wanajamii....TUJENGE PAMOJA.
 
hapo wamempiga, yaani gharama kubwa hapo ilikua nikutoa tu copy tena na yenyewe basi tu, kodi yetu inafanya kazi gani? kumpeleka tu mama salma dubai au?
 
Mhm? Ninavyojua mimi wizi ni kesi ya jinai.... Hapo mshtaki anakuwa jamhuri, na kwa kawaida huyo jamhuri ndo hushughulika na vinavyobaki. Mlalamikaji yeye hutoa taarifa, ushahidi na kuisaidia polisi(si kifedha)
 
Amepewa risiti? Kama anazo anaweza zipekeka takukuru kuulizia uhalali wake!
 
 
tatizo lao wanaendekeza njaa na rushwa sana. namshauri ndug yako awape za moto (takukuru),si bado wanampigia simu awapatie fedha za kumfuatilia mwizi. dawa ni hiyo tu.
 

kisheria samahani nduguyo nae mwizi..hizo hela za kugawa kapata wapi..???
 
Huyo ndugu yako ni mtega nyoka.....zatzwhy wamempiga.....mwambie ajitahidi kuwa mwelewa wa mambo
 
Vituo vyote vya Police ni kitovu cha rushwa. Shida yako ni mradi kwao. Wakiwa ndani ya jezi zao wanadhani wako juu ya sheria.
 
Pesa zote hzo mtu anakubali kutoa kirahisi rahisi,nahisi huyo ndugu yako alitaka kumbambikizia mtu kesi!
 

Kama kweli alifika hapo basi atapewa namba ya JALADA( kwa maana ukifungua shauri lolote polisi basi wanakupa namba ya jalada. Sasa kama unayo hiyo ingia kwenye web site ya Polisi tanzania kisha weka lalamiko lako hapo ukiambatanisha na hiyo namba kisha utaona itakavyo fuatiliwa.

Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…