British economist
Senior Member
- Jul 14, 2013
- 104
- 14
- Thread starter
- #21
Mtanzania amka, tafakari na chukua hatua
Nenda youtube andika Lipumba msikitini upate alichosema, siyo kubisha bila kuwa na data mkuu, ila ninachoweza kusema Ule ujinga aliousema Lipumba hakuna Muislamu anaweza kuushabikia, alidhihirisha tu kuwa hana uwezo wa kuwa kiongozi
mkinijibu maswali haya basi UKAWA wamepita na ni washindi ....
1. Wamegundua CCM ni noma, chama kimoja kimoja hakiwezi kuiondoa CCM Madarakani?
2. Zile tofauti za CHADEMA kulaumiana na CUF kuwa kila upande unaunga mkono USHOGA zimekwisha?
3. Kwa tamko hili ni dhahiri CHADEMA watalazimika kuunda bazara la mawaziri vivuli kwa kushirikisha vyama vinavyounda UKAWA, Je MBOWE ana uhakika wabunge wake wa CHADEMA watakuwa tayari kwa hilo?
4. LIPUMBA aliwahi kusema msikitini kuwa WAISLAMU wajipange na wao kutetea Mambo yao, kwa vile KIKWETE waliomchagua kuwatetea amewatosa, Je LIPUMBA atakubali kuona UKAWA wanamsimamisha Mkristo kugombea nafasi ya urais?
5. MPAKA SASA hakuna kiongozi wa juu kabisa NDANI ya UKAWA anayetokea Zanzibar, Je Wazanzibari watakuwa na imani gani na Rais atakayesimamshwa na UKAWA?
6.Endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa akitokea CHADEMA au NCCR-MAGEUZI na Zanzibar wakaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa kati ya CUF na CCM, hIzi serikali mbili zitashirikiana vipi?