Hii kauli ya Membe ameniacha hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii kauli ya Membe ameniacha hoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Jul 7, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kutokana wizi ulioripotiwa kutokea wizarani kwake, alipoongea na waandishi wa habari alisema "Haikuwa wizi bali ulikuwa ukiukwaji wa taratibu za fedha". Lakini wakati huo mkumbuke kuwa imeundwa tume ya kuchunguza ukwapuaji wa fedha hizo.
   
 2. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Unamshangaa Mwana CCM kutoa kauli ya hivyo?
  Rushwa wanaita Takrima
  Wizi unaitwa deal
  Mwenzao akiiba - Wanamtengenezea mazingira ajifiche ili raia wanyamaze.
  Mahakama zipo lakini kila tukio la wizi, ujambazi huundwa tume na majibu ya tume huwa ya utata.

  Hivi niulize labda ulikuwepo enzi hizo; alipouwawa Jenelali Kombe - tume iliyoundwa ilitoa majibu gani... ?
  Baada ya miaka kadhaa kupita walomuua si wako mtaani.

  ndugu yangu serikali tuliyonayo inawakumbatia waarifu ili walala hoi na waadilifu tuendelee kuteseka.
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Tutor nimekupata na hakika andishi lako limenikumbusha mambo mengi yaliyokwisha undiwa tume na majibu yakabaki kabatini mwa wakuu bila umma kutaarifiwa chochote.
   
 4. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kunapotokea jambo la kuitia serikali ya chama tawala aibu, huundwa tume, siyo kwa ajili ya kupata ukweli zaidi. Ila kwa matokeo ya tume nyingi, inaonyesha tume huagizwa zikaangalie namna ya kuzima malalamiko na kupindisha ukweli. Na huenda walalamikaji huitwa na eidha kutishiwa au kuhongwa ili wasiendelee kulalamika. Nadhani wapo pia walalamikaji wanaopotea kipindi cha uchunguzi wa tume. Kwahiyo ukiona tume imeundwa kaa CHONJO!
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni sawa na kauli ya Lipumba:"Msimtukane bure rais mkapa kuwa ni mwongo!!!Si mwongo bali ana tabia ya kutosema ukweli!!"
   
 6. r

  rugo Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu, mkisikia tume inaundwa kuchunguza jambo, mjue hapo tayari tumeibiwa. Kwa nn haikuundwa tume walipouwawa watalii, na baada ya siku mbili watuhumiwa wamekamatwa, lakini imeundwa tume 'Fasta fasta' tukio la kutekwa na kuteswa Dr. Uli
   
 7. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  wengine wangeambiwa wasijadili maana tume imeundwa!!
   
 8. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  membe huwa namwona mzushi tu. kuhusu meli za iran eti anasema ameomba uk na us wasaidie uchunguzi. kama wamesha chimba mkwara maana yake wanayo majibu tayari... huu si wehu
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..walikuwa wametenga 3 billion kwa ajili ya safari za Brazil,Swiss, na Arusha.

  ..Membe ana maelezo au utetezi gani kwa matumizi makubwa kiasi hicho??
   
Loading...