Hii kauli ya Makamu wa Rais ifanyiwe kazi haraka

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,406
Nimemsikia makamu wa rais akisema kuwa kuna watoto wa shule wanajiuza kwenye clab za usiku, hili jambo sio la kupuuzwa hata kidogo, wazazi wanatumia fedha nyingi kuwalea watoto na kuwagharamia ki masomo halafu wakafanye biashara za hovyo hapana.

nilitegemea kabla ya kauli hiyo tayari watoto kadhaa wawe wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano, hizo kumbi zina camera za usalama uongozi wa chuo husika waende kutizama na kubaini wanafunzi tajwa. najua mkuu huyu aliyasema hayo akiwa na ukweli usiokuwa na shaka kwani anavyo vyanzo mbalimbali vya habari yaani ndio mwenye dola na dola ina mkono mrefu.

ni wakati sasa wizara husika iweke kanuni kuwa chuo kidahili wasichana kulingana na uwezo wa mabweni waliyonayo ili watoto wa kike wote wakae bweni tena chini ya uangalizi wa matron. Haingii akilini chuo chenye uwezo wa kuwapatia malazi wanafunzi elfu mbili kudahili wanafunzi elfu sita hapana hizo ni tamaa za fedha hakuna sababu chuo kudahili wanafunzi wengi zaidi ya uwezo wake.

Mwanafunzi akae nje ya chuo kwa sababu maalumu, labda awe ananyonyesha au ni mke wa mtu, mfano wanafunzi wa masters anaweza kuwa ni mama mtu mzima mwenye familia huyo anaweza kaa nje ya chuo.

Zipo clab za usiku hutuma magari kusomba mabinti wa chuo kuwapeleka kwenye disco na dansi za usiku hili lipigwe marufuku, miaka ya nyuma madisco ya wanafunzi yalikuwa yakifanyika maeneo ya chuo sasa hili la akina sumaye kuwakusanya watoto katika kumbi za usiku kwa kisingizio cha mafahali hapana hatuwezi kubaliana nayo lazima maadili yazingatiwe.

Ukweli ni kuwa sasa hivi watoto wanaanza shule wakiwa wadogo muda mwingine mtoto anaanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka mitatu na anarushwa darasa hivyo upo uwezekanao akahitimu chuo kikuu akiwa binti mdogo na asiyejitambua.

Tuliwahi sikia sintofahamu ya mwanafunzi aliyekuwa akiishi na hawara kibaka bwenini tena asiyekuwa mwanachuo. Hivyo hii kauli ya makamu wa rais lazima ifanyiwe kazi na kutolewa ufafanuzi.
 
Mukandara akipita hapa atawaomba mods wakugonge ban za kutosha.



Chuo chake ⅛ ya wanachuo ndo wanakaa hostel
 
Wale wa Dodoma waliowafukuza usiku na mbwa wa polisi hawakujua kuwa hata wao wangeweza kujiuza ili wapate pa kulala? Waache maigizo kwani hawana huruma yeyote na mtoto wa masikini, hawana kabisa
 
Eti " ni wakati sasa wizara husika iweke kanuni kuwa chuo kidahili wasichana kulingana na uwezo wa mabweni waliyonayo ili watoto wa kike wote wakae bweni tena chini ya uangalizi wa matron" Hicho bado kitaitwa chuo kikuu kweli au ni Shule ya sekondari? Halafu mbona unaangalia upande mmoja tu wa wanafunzi i.e wa kike tuu? Hujasema kama na wanafunzi wavulana wanaotoka chuoni kwenda kwenye hizo kumbi za starehe za usiku kupata huduma hizo za dada poa nao waleleweje. Shida yetu tunataka kurudisha mshare wa saa nyuma wakati muda unasonga mbele.Tatizo hili haliwezi kutatuliwa na polisi au kuwalinda wanafunzi kama fedha benki bali kwa kuwapa watoto wetu malezi bora yanayozingatia maadili na nidhamu ya kumcha mungu tangu wakiwapo nyumbani na wawapo mashuleni.
 
Back
Top Bottom