Hii kasumba tutaacha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii kasumba tutaacha lini?

Discussion in 'Sports' started by dazu, Jun 11, 2011.

 1. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuna kasumba mbaya sana ya kudharau vyetu na kutukuza vigeni tukiamini ni vizuri kuliko vyetu. Mbaya zaidi sasa hivi hata viongozi nao wanayo hii kasumba. Mwaka 1980 tuliposhiriki kwa mara ya kwanza na ya Mwisho AFCON tulikua na makocha wazalendo akina Joel Bendera. Mwaka 1993 tuliponyakua kombe la Challenge Timu yetu ya Taifa iliongozwa na wazalendo akina Mziray na Mkwasa. Serengeti boys ilipofuzu Africa miaka michache iliyopita (Kabla ya kuondolewa kwa kumchezesha Nurdin Bakari aliyedaiwa kuzidi umri wa miaka 17) ilikua na wazalendo akina Abdallah Kibaden na Sylivester Marsh. Mwaka huu Mzalendo mwingine Julio amekabidhiwa Ngorongoro Heroes, na mwendo wao tunauona kwenye kufuzu olyimpic, maana ni kama wametanguliza mguu mmoja kufuzu.


  Inasikitisha Naibu waziri wa michezo haoni mchango huu wa wazalendo badala yake anaendeleza kasumba ya kupenda vigeni, na kumvunja moyo Julio kwamba Serikali ina mpango wa kutafuta kocha wa 'kigeni' katikati ya mafanikio haya ya mzalendo. Hivi kocha wetu lazima awe mgeni? Tujiulize Maximo amekaa miaka mitatu, kila siku tunapewa matumaini "Tumpe muda" huku analamba mshahara kibao. Fikiria tangu aondoke mpaka sasa hajapata timu ya kufundisha. Sasa amekuja Poulsen, hatuwezi kusema ndo kaleta kombe la challenge maana amekuta vijana walishaandaliwa. Mwenendo wa Timu yetu tunauona katika mashindano ya kimataifa. Nadhani kuna haja ya kujikomboa kifikra na kuamini kwamba Watanzania wanaweza pengine kuliko hao wageni wanaowachukua.
   
 2. M

  Masuke JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  hata mimi nilimskia nikasikitika sana, sijui hawa viongozi wetu wana nini.
   
 3. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Ndivyo walivyolelewa na wazazi wao kuabudu vya nje, huoni hata JK tabia yake ya kitumwa hawezi kuacha.
   
 4. P

  Pazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Labda tunarisi ya wakoloni wa Uengereza.... Haya Matatizo ndio wanayo Britain ya kutaka Ma Manager wao na kupondana kwenye magazeti au Kusifu timu ya Taifa alafu ikifungwa Game Moja kila mtu anarukia Manager wa nje hafai wanataka wao, ndio sie sasa tabia zilezile... Mie Sipingani na Ma Manager wa Nje ila kwa uchumi wetu hatuna uwezo wa kupoteza Pesa kwa Mafundi wa Nje bora pesa zibaki kwa Mafundi wetu... Julio kwa maoni yangu ni fundi mzuri sana anawapa moyo vijana wengi na anajuwa nini anafanya na habagui kuhusu wachezaji timu gani kubwa anacheza anachaguwa kipaji na anajuwa matatizo ya vijana na makwao kwenye familia zao hilo ndio muhimu kwa fundi mzuri wa michezo.
   
Loading...